help: mganga wa kienyeji mbagala

help: mganga wa kienyeji mbagala

newbie

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
216
Reaction score
48
poleni na majukumu wanaJF kwanza kama hapa sio jukwaa sahihi mods naomba mnisaidie, nimeona kwenye gazeti la nipashe kona ya matangazo madogo madogo kama unatafuta dawa ya kumrudisha mume,mke au mpenzi,dawa ya mvuto,kupandishwa cheo kazini na kadhalika. yale matangazo huwa ni mengi ukurasa mzima sasa nikachukua namba moja wapo nikapiga jamaa akafanikiwa kuniconvince kuna dawa atanipa ya kunifanya niheshimike kazini na niwe na mvuto bei ni 60,000 nikamwambia nina 40,000 akasema poa nyingine nitamalizia baada ya kuona matokeo. sasa masharti yake naona siyaelewi mara nikioga nayo nimpigie simu ili aniunganishe na maruhani yake mara nichukue hela nyingine niweke kwenye maji yenye hiyo dawa,etc sasa sitaki tena hii mambo JE NAWEZA KUPOTEZEA TU AU NITAPATA MADHARA? am just worried what will happen nikiendelea kufanya mambo yangu,ananipigia simu kila saa sipokei. nisaidieni mawazo wadau
 
Mkuu.@newbie sasa wewe umekwenda kwa huyo Mganga hujafanya hiyo Dawa ?au umeshafanya? unatuachanganya mbona maneno yako? Kama umeshaanza hiyo Dawa maliza kabisa hiyo dawa kuifanya uone matokeo yake, kisha uje hapa utupe Feedback. Timiza masharti ya mganga kisha uone matokeo yake mbona unajitia wasiwasi Mkuu? Tena huyo amekuchaji bei ndogo tu ningelikuwa ni mimi ingelibidi utoe TZ Shs Laki 1.
 
sijakwenda kwake kwasababu nakaa mbali tulikutana tu sehem akanipa kwnye kimfuko,ni unga unga fulani.
tatizo sio kutumia bali ni huko kuniambia nimpigie simu kuongea na hayo maruhani. swali langu ni kwamba ARE THESE THINGS FOR REAL?
 
Mkuu newbie if you want know that is real try it, then give me feedback.
 
Last edited by a moderator:
we achana na huo upumbapfu kabisaaaaaaaa mpaka leo unatapeliwa kizembe hivyo.basi kwa hilo we mtegemee mungu tu utakuwa salama.hapo alikuwa anataka akufilisi kwa kuzivuta hizo pesa na sasa ashindwe kabisaaa
 
thanx mkuu,nimeogopa labda nikitupa hii dawa yake nitadhurika
 
Back
Top Bottom