Helpless:...My Dad's Gone!

.......Pole sana kwa kufiwa na baba Pakajimmy
Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe.
 
Mkuu pole sana najua hali uliyoko nayo hivi sasa, Naamini Mungu atakupa nguvu upite wakati huu salama. Tuko pamoja kwa siku hizi mpaka tumsafirishe mzee wetu katika safari yake ya milele.
 
RIP mzee wetu,pole PJ.NASHAURI IKIWEZEKANA IFUNGULIWE THREAD YA MCHANGO WA RAMBIRAMBI KUTOKA KWA WANA JF ILI KUMSAIDIA NDUGU YETU PJ.
Tunatofautiana kwa hoja but all in all sisi wote ni ndugu i mean wabongo.
AMEEN
 
Pole kwa Kufiwa na baba PakaJimmy,
Mwenyezi Mungu akupe nguvu, usafiri salama na shughuli za msiba ziishe salama.
 
Ni tukio kubwa, hutokea mara moja kwa watu unaowapenda na halina uzoefu.
Pole sana PJ Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu, maisha yetu kama binadamu huu ndio mtihani wa kuishi kwetu pole sana!!
 
pole sana.
hard times makes a man.be strong.
pole sana.
 
Pole sana mkuu nadhani utafanikisha mambo vizuri kabisa bila matatizo!!
 
Pole sana kwa msiba. Binadamu sote ni mavumbi na mavumbini tutarudi. Ni njia yetu sote.
Mungu azidi kukutia nguvu na kukufariji.
 
Pole mkuu.RIP our dad. mkuu ila ujue kuwa ukienda bongo hata kama ni kwa matatizo utapigwa mizinga kama kawa. mimi niliexperience this before last year when i losted my beloved mom.
so mkuu tuko pamoja i know it pain .yaani we omba tu usikie kwa wenzio but when it come to u you will never believe.pole sana bro GOD is with u.
 
Wapwa na mabinamu kama kawaida yao, wapo wanajipanga kuelekea eneo la tukio kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu mida ya saa sita. Kwa wale ambao waajiri wametutaiti kwa siku ya leo ndo hivyo tena tunabaki kuwasiliana na wapwa na kuripoti hapa.
 
Mkuu PJ pole sana, mungu awatie nguvu kipindi hichi kigumu kwenu.

Bwana alitoa na bwana alitwaa jina la bwana lihidimiwe
 
Pole sana PJ. May the Almighty give you strength and courage during this difficult period.
WanaJF, nakumbuka sana upendo ulioonyeshwa na PJ wakati Sipo alipofiwa na babu yake. Nina imani wanaJF walioko Arusha, Dar na Mbeya (na kwingineko), ambao wataweza, watatuwakilisha katika msiba huu. Nasi tulio mbali tuko nanyi kiroho.
Natoa shukrani za awali kwa wote watakaoshiriki.
RIP baba PJ.
 
"Mimi ndimi huo ufufuo na uzima, yeye aniaminie mimi ajapokufa atakuwa anaishi" Yoh. 11:25

PJ - huu ni msiba mzito na mkubwa sana, namuomba Roho Mtakatifu akupe nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu. Na Mungu wa amani yote ailaze roho ya Marehemu mzazi wako Mahala pema peponi... Amen

Wana JF, nimefurahishwa na solidarity ya members wote... ingawa wengine hatuwezi kushiriki kimwili lakini rambi rambi tunaweza kutoa ili iweze kusaidia katika msiba. Tafadhali tufahamisheni rambi rambi zetu tuwasilishe wapi. Msiba una mahitaji makubwa sana, tungependa kusaidia

Respect
 
tupo pamoja! wakuu
leo ndio nimerudi ofisini baada ya kuhakikisha rafiki yetu pj anapata support ya uhakika!

ameniomba niwashukuru sana woote walio guswa na swala lake

wapo waliompigia simu,wapo waliochangia michango yao kutoka sehemu mbali mbali za nchi,

kwakweli pj amewashukuru sana!alipata faraja kubwa sana baada ya kuwaona jf-members katika kipindi chake kigumu...
 

tunashukuru sana mkuu!tupo pamoja JF WOTE!...kama unataka kutoa michango naomba uni-piemu.kuna michango mingi ya pj ipo chini ya uangalizi wangu mimi na JS AMBAYO TUNATARAJIA KUMKABIDHI PINDI ATAKAPORUDI...!

ahsante
 
pamoja hommie!....
naamini alikupigia pj..!kimsingi anatamani sana kukufahamu.ANASHUKURU SANA!

TUPO PAMOJA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…