Makbel
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 774
- 167
Hongereni HELSB kwa kuendelea kutunyima mikopo sisi ambao tuliomba mwaka jana na kutunyima na tumekata rufaa pia rufaa zetu zikatupwa bila kutolewa maelezo. Tumejaribu mwaka huu tukiwa na attach zote kutoka vyuoni lakini cha kusikitisha bado tumekosa hiyo mikopo. Sasa basi hizi lawama za sisi kuendelea kupata maambukizi ya Ukimwi mavyuoni kamwe hamuwezi kuziepuka kwa sababu ya haya mnayotufanyia kwa kutunyima mikopo wakati ni haki yetu kikatiba kwa sisi tusio na uwezo wa kujilipia ada. Hatujui hatma ya maendeleo yetu vyuoni tunavyosoma kwa sasa maana maisha ya vyuoni na gharama zake ni balaa sana. Mwisho tunaomba mtuambie sisi ambao mmetunyima mkopo kwa first year mwaka wa masomo 2012/2013 hatuna haki ya kupata mikopo tena kwa miaka iliyobakia ya masomo? Nimeuliza hivyo maana hatuoni sehemu yetu maalum ya kujaza fomu za OLAS kwa sisi tuliopo vyuoni na hatuna mikopo na tunaomba sawa sawa na first year wanaotarajiwa kuingia vyuoni. Bila shaka mmemielewa na mtafikiria kuwa na sisi ni Watanzania tunaostahili kukopeshwa na si hivi mnavyotufanyia. Ni mimi Afiswa Amir Ngayana kutoka Muslim University of Morogoro. P0728.0001.2001