Hemed Morocco hatoshi kuwa Coach wa Taifa stars AFCON

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Najua Watanzania ni watu wa matukio
Hapa tumefuzu Kwa mbinde na coach Morocco anaonekana shujaa, ila ana mbinu duni akikutana na timu ngumu atapigwa kama ngoma

Tumefuzu lakini Kwa kubahatisha tu
Huko AFCON tunaenda kutia aibu
Tutafungwa magoli si chini ya 5 kila mechi

Timu yetu inacheza kama haina coach

Timu inacheza Kwa hamasa tu
Timu haina muunganiko
Coach Morocco hawezi ku manage wachezaji, ashawahi kugombana na wachezaji wengi akiwemo Dickson Job, Msuva, Samata, Haji Mnoga, Mmobwa n k
TTF tafuta coach mwingine
Muda upo wa kutosha
Msiwe na mihemko wa ushindi wa kufuzu Kwa mbinde

Wasaalam
 
Uwezo wa wachezaji ni mdogo mno
 
Timu yetu inahitaji kocha mzawa sababu karibu 90% ya wachezaji ni wa ligi kuu. Nashauri wamchukue Gamondi kabla hajapata timu nyingine, atleast anawajua wachezaji wa bongo.
We jamaa hata hujui ulichoandika. Timu yetu inahitaji mzawa hapo hapo unashauri apewe Gamondi...Huyo Gamondi ni mzawa? Au mmeambiwa kuna stars inatumia sindano?
 
Timu yetu inahitaji kocha mzawa sababu karibu 90% ya wachezaji ni wa ligi kuu. Nashauri wamchukue Gamondi kabla hajapata timu nyingine, atleast anawajua wachezaji wa bongo.
Gamondi si type ya national team coach, so akija ni kama anajiua kiwango
 
Kwahiyo akija Klop tutachukua kombe?
 
Wewe ni zwazwa,, bendera fata upepo,,,,, ! Stars imeshinda umeishobokea sio,,,unakuwa kama malaya alieona wallet!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…