Hemed Moroco sijui nini Taifa stars kocha ang'olewe ama atatufikisha AFCON ijayo?

Huu ni upumbavu!
Katika timu 16 wachezaji wageni ni wangapi?
Hawa wachezaji wenyeji unaowapambania kwa nini hawaoneshi uwezo kwenye hizi timu za kawaida?
 
Sina hakika sana km uwezo uwezo wa Moroco unaendana na MALENGO na MATARAJIO ya Taifa
 
Tafuteni kocha achaneni na huyu tapeli.
 
Kiukweli TFF kama Taifa stars itashindwa kwenda morocco tutawashika matamvua yenu huwezi kumpa timu Hemedi Moroko halafu utegemee aipeleke Afcon , hata ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania hajawahi kuubeba.
 
bora hata meci mexime ambae amewahi kucheza timunya taifa na kuwa kepteni,wakati wa marcio maximo,au hata bakati shimye
 
Hemed Morocco pale amewekwa na yule mshikaji wake mzanzibar ambaye ni mkurugenzi wa ufundi pale tff
 


Hamna kocha humo
 
Huna hoja
 
Umeniwahi mkuu,,ila hata mimi nilikuwa nawaza hili

Imekuwaje hemed Morocco akawa kocha stars?
Kwa kipi kwa mfano?
 
Mechi za kufuzu ni 6 tu.
Nyumbani mechi 3, Ugenini mechi 3.

Mechi nyepesi kuliko zote, kimtazamo wa haraka ilikuwa hii ya nyumbani dhidi ya Ethiopia...

Sasa Tunaenda ugenini Guinea tukiwa frustrated kwasababu ya Ujuha wa kocha wetu.

Mimi siamini kama kocha Hemed Moroko alikuwa na dhamira ya dhati ya kupata alama 3 nyumbani....

Uzembe wa kipuuzi wa mtu mmoja unaligharimu Taifa..

Tulicheza friendly mechi na Bulgaria, Mongolia na Indonesia hivi karibuni,

Hizo zilikuwa mechi sahihi kwa kocha kufanya majaribio hayo aliyoyafanya kwa Ethiopia ya kutumia mabeki 6!
Ukiwa nyumbani kwenu na ukihitaji kushinda.
 
Huyu kocha kwa CV yake ilivyo, kuwa kocha wa timu ya taifa ni aibu na dhihaka kwa wapenda football!
Kocha kafundisha Namungo hata top 10 ya ligi haikufika, na iliyoponea kushuka daraja, hata kuongea kwenyewe kwenye media hayui! Mnatutesa sana wapenda mpira yan!
 
naunga mkono,hajui kuongea na anababaisha tu kuongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…