Hemed Seif: ''Inside 10" Nyota wa Gossage na Challenge Cup

Hemed Seif: ''Inside 10" Nyota wa Gossage na Challenge Cup

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HEMED SEIF: ''INSIDE 10'' NYOTA WA GOSSAGE NA CHALLENGE CUP

Hayo maneno hapo chini nimeyatoa katika taazia niliyomwandikia Hemed Seif alipofariki dunia mwaka wa 2014.

Hizo picha nimeziweka kuanzia 1958, 1961, 1965 akiwa katika timu ya Tanganyika.

Picha ya mwisho nilimpiga Tanga akiwa katika utu uzima lakini akipata nafasi anakwenda kucheza mpira viwanja vya shule ya Popatlal:

''Mwaka 2000 nilikwenda kufanya kozi Nairobi na mmoja wa walimu wangu alikuwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Mohamed Abdilkadir.

Alipojua natokea Tanga akaniuliza kama namjua Hemed Seif.

Nilipomweleza kuwa Hemed Seif nikonae barazani kila siku na tunafanya kazi pamoja bandarini alifurahi sana ndipo akanipa kisa chake kuhusu Hemed Seif.

Alinambia kuwa yeye katika miaka ya 1960 alikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Nairobi na alikuwa akicheza timu ya taifa ya Kenya akiwa katika safu ya ulinzi kama ''half back.''

Anasema siku ilipojuliikana kuwa Kenya watakutana na Tanzania, kocha na wachezaji wenzake walimuonya kuwa awe makini sana na Hemed Seif, amwangalie sana asimuachie hata kidogo kwani ni mfungaji mabao hatari mno.

Mohamed Abdilkadir anasema ikawa sasa kwake ni vitisho wenzake wakimtisha kwa kumpigia makelele, ''Mohamed, Hemed Seif huyo nyuma yako...''

Basi katika mazoezi ikawa ni vicheko na vitisho kwake kuhusu Hemed Seif na mashuti yake.

Maelezo haya yakanitia hamu nikamuuliza nini kilitokea Nairobi City Stadium siku ya mechi ya Kenya na Tanzania.

Mohamed Abdilkadir alitingisha kichwa akasema,''Bwana ilikuwa kazi.

Mimi nilimpania Hemed Seif.
Sikuwa nabanduka nyuma yake.

Nilikuwa kama kivuli chake, kila anapokwenda niko mgongoni kwake...wapi bwana.

Kama walivyonitahadharisha wenzangu kitambo...
Hemed Seif alifunga bao kama kawaida yake.

Nikakumbuka maneno ya wachezaji wenzangu kuwa Hemed Seif hatoki uwanjani bila ya kutingisha nyavu.''

Hemed Seif alikuwamo katika timu ya Tanzania ilipocheza na timu kali ya daraja la kwanza kutoka Uingereza, West Bromwhich Albion ilipokuja nchini na kucheza na timu ya Tanzania Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru).

Kama kawaida Hemed Seif aliwatoka mabeki wa West Bromwhich na kufunga goli.

Picha yake ilitoka kwenye ''Tanganyika Standard'' ikimuonyesha Hemed Seif akifunga bao hilo.

Huyu ndiye Hemed Seif aliyekuwa msakata kabumbu maarufu.

1665255085637.png
1665255123249.png
1665255144365.png
1665255171346.png
 
Miaka ya sitini alikuwa striker hatari wa klabu bora nchini TPC ya Moshi Basi wakija kucheza na Arusha combine Hemed kwake hat trick ilikuwa kitu cha kawaida
Palikuwepo mid fielder mzuri sana aitwaye Sembwana na pia Mbwana Mtoto
 
Back
Top Bottom