Hemedy "kina dada mniache sitaki kufuatwa fatwa mmenisumbua kwa kipindi kirefu"

Hemedy "kina dada mniache sitaki kufuatwa fatwa mmenisumbua kwa kipindi kirefu"

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
STAA wa filamu za Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, amewataka kina dada wanaomtaka mahusiano ya kimapenzi kukaa mbali naye, kwani kwa sasa ameamua kutulia na mpenzi wake, na anatarajia kufunga ndoa.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, PHD aliandika kuwa kwa sasa yupo tayari kumweka hadharani mpenzi wake, ambaye anatarajia kufunga naye ndoa hivi karibuni, hivyo hataki kufuatwa na wasichana ambao hawapendi maendeleo yake.

“Nimekuwa nikisumbuliwa sana kwa kipindi kirefu, hata mimi pia nimewachezea sana watoto wa watu, sasa nimeamua kutulia na kuwa mwanaume bora, maana nimegundua nilikuwa nafanya ujinga, umri ushaenda, natakiwa niwe na familia yangu,” aliandika.
Mbali na hilo, PHD alisema yupo katika hatua za mwisho za maandalizi ya video ya ngoma yake mpya anayotarajia kuisambaza mwezi huu inayojulikana kwa jina la ‘On My Wedding Day’.
Alisema katika wimbo huo, amezungumzia mambo mengi ambayo anatarajia yatakuwepo siku yake ya harusi, hivyo anaomba sapoti kwa mashabiki ili iweze kufanya vizuri.
PHD ni kati ya nyota wa Bongo wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu na muziki, kutokana na ubora wa kazi zake na anavyoweza kucheza uhalisia mbele ya kamera.
 
ambae hataki kufatwa fatwa huwa hasemi semi ovyo he just act

zaid anatafuta attention tu
 
Angeamua kukaa kimya tu sijui angepungua kitu gani, hao ndio mastaa wetu wa nchi yetu
 
Muuzasura wapiii njoo utuambiee huyu anafatwafatwa na kina kaka au kina dada!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Aache na kuvaa hereni..Ni ujinga pia..
 
Hapo ndo utaona utofauti wa mwanaume na mtoto wa kiume ,Diamond yuko busy kusafiri kusaka fedha ,mtoto wa kiume hemed yuko busy kutafuta attention za mapenzi,
Poor you halafu kwakua nakaa mtaa mmoja na huyu mtu namuona kama kichefuchefu hata buku la vocha anagongea
 
Hapo ndo utaona utofauti wa mwanaume na mtoto wa kiume ,Diamond yuko busy kusafiri kusaka fedha ,mtoto wa kiume hemed yuko busy kutafuta attention za mapenzi,
Poor you halafu kwakua nakaa mtaa mmoja na huyu mtu namuona kama kichefuchefu hata buku la vocha anagongea
anagongea kwa nani sasa..! si mlisema ana urafiki na shabiby..:confused3:
 
Kwani huyu yoyoo nae ni mzuri mpaka afwate
 
Back
Top Bottom