Mwenyekiti Mtendaji wa Britts Events, Awin Williams Akpomiemie Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Awin Williams Akpomiemie ameeleza kwa kina katika maelezo ambayo Bongo5 tumeyatafsiri kwa Kiswahili hapo chini. Watu wangu awali ya yote, ningependa kuelezea moyo wangu kwa kuuambia umma na mashabiki wa Diamond Platnumz, kwamba sisi kutoka uongozi wa Britts Events tunaomba radhi kwa kile kilichotokea usiku uliopita, wakati wa show ya Diamond Platnumz. Haikuwa imepangwa show ichelewe kuanza au kwa msanii kutotumbuiza. Hapa ntawaeleza ukweli wote wa kile kilichotokea katika tamasha hilo kwakuwa ninyi nyote mnataka kuujua ukweli. Mradi wa Diamond ulikuwa wa gharama kubwa sana kwakuwa uongozi Britts Events ulitaka kila kitu kiwe professional. Kama kampuni tuliamua kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye mradi huu hivyo tuliwafuata wawekezaji watatu lakini mmoja wao hakuwekeza sana kwani alidai hatokuwa nchini. Wawekezaji wawili ni watu wanaofahamika sana jijini Stuttgart, mmoja anafanya kazi na jeshi la Marekani na mwingine anamiliki kampuni ya usafirishaji mjini Stuttgart. Hawa ndio wawekezaji wakubwa tuliowapata. Tuliwapa mikataba wasaini lakini yule mwenye kampuni ya usafirishaji alikataa kusaini mkataba wa mradi huo kwakuwa alitaka kuwa na mkataba wake binafsi na yule jamaa wa Marekani. Kisha nilimwambia Mr.USA kuwa hiyo haikuwa hatua sahihi lakini Mr.USA alisema Britts msiwe na shaka, kila kitu kitakuwa poa. Watu wangu, mradi ulianza na kisha wale wawekezaji wawili wakagundua kuwa Diamond ni msanii mkubwa na angevuta umati mkubwa wa watu na watu wanampenda. Kisha walijiunga pamoja dhidi ya Britts waliowaalika kama wawekezaji kwenye mradi huo na walitaka kuuchukua kutoka kwa Britts sababu ni wao ndio walioleta sehemu ya fedha kwaajili ya mradi huu wakati Britts ndio wanaommiliki msanii na mradi wenyewe. Ila tu kwakuwa Britts ni kampuni mpya mjini Stuttgart, Mr. Shipping Guy aliamua kuungana na yule jamaa wa Marekani na DJ Wanted, kuuchukua mradi. Pindi Britts ilipokaa chini na kufanya mkutano nao, walikuwa wakifanya mkutano wao wenyewe na kubadilisha mipango yote hivyo walikuwa wanahujumu na kuendelea na mradi nyuma ya Britts. Britts ina makubaliano nao kuwa pindi msanii atakapowasili Ujerumani, watampa balance ya 3.250 euros, na walikubaliana na kigezo hicho kwasababu Diamond aliweka wazi kuwa bila fedha asingepanda ndege. Waliniomba mimi niongee na Diamond kuwa watampa fedha kwenye uwanja wa ndege, lakini unajua nini? Kabla Diamond hajawasili Mr. USA na Mr. Shipping