Sijui, nadhani ni ngumu kupata jibu muafaka. Jaribu kufikiria kuhusu waMasaai, waMang'ati n.k. makabila ambapo kuvaa hereni ni sehemu ya urembo kwa jinsi zote!
Ila kusuka...mh!
<br />mwanaume anayevaa kihereni hata simuelewi,hakuna cha utamaduni wala nini,hereni za masai na wamangati zinaeleweka na zinakubalika lkn ni tofauti ni hizi wanazovaa makaka zetu wakimjini.<br />
mbali na hereni,mwanaume anayevaa mipete mingi,anayesuka nywele,anayefuga afro,anayeweka wave,huwa simuelewi.<br />
kuna wakaka wanapaka wanja kwa mbali na lipgloss,kuna mmoja sasa hivi ameoa aliniombaga rangi yangu ya kucha zile colorless zile zenye rangi kama ya maji zenye kungarisha kucha,nikampa nikidhani anatania duuh sikuamin jamaa ikajipaka kweli, nilishangaa.<br />
wakaka mkizidisha ubitozi wakijiremba mkibashiwa msilalamike.
Kama ingelikuwa ni kutoa maksi, basi mwanaume akivaa hereni au kasuka nywele, mimi nampa sifuri!
Mhhhh! Madame KH! kwako ni MARUKUFU kuvaa hereni na kusuka nywele!....Yaani huangalii chochote kingine! ali mradi ana nywele za kusuka na hereni basi anapewa mzinga! na yule mwenye mkufu wa gold lakini hajasuka wala kuvaa hereni je atapewa hata pass marks za kumvusha tu? Mzima KH? mbona umepotea hivyo!? Vibaya hivyo! haya uwe na weekend njema na pia ubarikiwe kwa sana tu.
BAK, yaani kabisa..anapata sifuri. Inabidi iwepo tofauti kati yangu na yeye...sio kila asbuh tunakuwa busy wote kujiremba..hahaha!
Kwa mkufu, mhh may be anaweza kupata some maks, ila sijui hata zitafika pass mark....🙂
Mi mzima kabisa BAK, mzima wewe? Nitajitahid kutopotea sana...
Hapari wapendwa!
Poleni na mihangaiko ya hapa na pale
tumekuwa tukichangia hoja za hapa na pale, zaidi kuna uzi mmoja hivi tulikuwa tukiuchangia kuhusu suala la wanawake kuvaa wigi, kila mmoja ni shahidi jinc watu walivyochangia/kupinga.
Sasa leo naomba mchango wenu kuhusu suala la wanaume kuvaa hereni na kusuka kama wadada!
Hivi hii ni akili au upunguani?
Hii ndo kwenda na muda au ndo kuchanganyikiwa?
He he he mi nadhani inategemea tamaduni na kazi ya mtu..wamasai wa kiume mbona wanasuka...ila @ least uwe na mwili wa gym na ndevu kidogo usije ukapapaswa bure
Hapo nakupata, sio siri element za kuchora 7 zipo, inakuaje mwanaume uvae hereni kama za dadaako, usuke nywele ka mamaako afu ujiite dume?
Tuachane na zile za asili kama za wamasai ambao huvaa hereni wakiwa ndani ya mavazi yao ya asili, sasa we haupo kwe asili afu umetoga masikio, nyusi, nk mfn Aliekuwa mtangazaji wa EATV Ben K. Sasa ile ni asili au ni nini?
hakuna kitu nachukia kama mwanaume kuvaa mikufu
nachukia zaidi pale anapovaa HERENI
Halafu nachukia na kukasirika pale wanapovaa MILEGEZO
na huwa nanuna nikiona wanaume wakitembea barabarani na vikaptura mpaka "maumbile" yao yanayowasababisha kuitwa wanaume yanapojichora kama yalivyo kwenye hivyo vikaptura !!!
yaani nachukia nachukia nachukia.....
natoka kwa sasa... nitarudi kumalizia!!!!!!!!
mi mzima,
hao wanaovaa pichu nje ndo natamanig niwanyuke viboko,nahis wanawatega wanaume wenzao maana unakuta wakipita wanaume wenzao wanakodolea macho.hii dunia imechefuka sana
Avatar yako mbona inanitia wehu mie? Na nyie jamani wanawake acheni kututega kuvaa nguo zinazobana makalio hujui tunaumia sisi?
we kwan mada ni avatar au heren?