zephania5
JF-Expert Member
- Aug 18, 2022
- 232
- 807
Awali ya yote, nipende kumshukuru Mungu mwenyezi atupae uhai na uzima bure, pamoja na afya kwa wana jamii forum wote. Afya njema iko juu ya mali na utajiri. Afya bora ni zaidi ya umaridadi au umashuhuri, na tena afya ni zaidi ya kutokuwa na ugonjwa. Zipo tafsiri mbalimbali juu ya afya ikiwemo ile ya shirika la afya duniani(WHO) ya mwaka 1948 inayosema '' Afya ni hali ya ustawi wa kimwili, kiakili, kijamii na sio tu hali ya kutokuwa na ugonjwa au udhaifu wa kimwili na kiakili''. Afya ni zaidi ya kutokuwa na ulemavu. Afya njema humweka mtu mbali na magonjwa au maambukizi, pamoja na athari zinazoletwa na magonjwa. '' Nilipokuwa kijana mimi na afya tulitafuta pesa, na sasa nimezeeka, mimi na pesa tunaitafuta afya'' Aliwahi kusema mzee mmoja. Ni kweli kuwa umaskini kwa kiasi.
Karne ya 21 na fya
Kila kitu tunachokifanya kina athari juu ya afya zetu, ikiwa ni athari ya moja kwa
moja au isiyo ya moja kwa moja. Kila kitu tunachokula kina athari ndani ya miili
yetu, mara nyingi afya zetu zinaathiriwa na chaguzi za kila siku yaani ule nini, unywe nini ama ufanye nini! Kwa miaka ya hivi karibu katika zilizoendelea pamoja na nchi zinazoendelea mazingira yanayotuzunguka yamegeuka kuwa adui kwa afya ya binadamu. Julai 18 2022, homa ya mgunda(Leptospirosis) ikathibitishwa rasmi kimaabara hapa nchini Tanzania, chini ya wizara ya Afya.
Chanzo hasa ikiwa ni mwingiliano wa maji pamoja na mkojo, kinyesi kutoka kwa wanyama wa kufugwa na wanyama pori. Usalama juu ya afya ya binadamu umekuwa ni mdogo sana, maana hata binadamu wanaomzunguka nao kwa kiasi kikubwa husababisha magonjwa na kudhoofisha afya pia. Magonjwa kama kifua kikuu(TB), pumu na homa ya ini( Hepatitis B) ni moja ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa kasi kutoka mtu mmoja kwenda kwa mtu.
Mwingine kupitia njia ya hewa pamoja na kugusana. Magonjwa mengi yanayohusiana na mfumo wa upumuaji kama saratani ya mapafu, yanachangiwa pia na wimbi la ongezeko la ongezeko la vyombo vya usafiri kama.
Magari, pikipiki, na treni au magari moshi vinavyotoa hewa chafu na kuharibu anga hewa. Ongezeko la viwanda na maendeleo ya sayansi na teknolojia, yamekuwa na manufaa kwa maisha ya kila siku kwa mwanadamu, lakini kwa upande mwingine yamekuwa na madhara makubwa katika uchafuzi wa vyanzo vya maji, uchafuzi wa ardhi, uchafuzi wa angahewa pamoja uharibifu wa mimea, na hivyo kuhatarisha afya
ya binadamu kwa namna moja au nyingine.
Inawezekanaje kuwa mwenye afya njema?
Kwa kiasi kikubwa afya ya mwanadamu
huatambatana na dhana ya kwamba: nini anapaswa kufanya na nini hapaswi kufanya ili aendelee kuwa mwenye afya njema, pia ni nini anapaswa kula au kunywa, na ni nini hatakiwi kula au kunywa ili awe salama katika afya yake. Yapo mambo kadha wa kadha yanayoweza kumsaidia binadamu kuepuka kutembelea vituo vya afya, au
kumuona daktari mara kwa mara, maana kinga ni bora kuliko tiba.
1.Chakula bora chenye afya njema.
Eating healthy during a pandemic
Si kila kinachoingia tumboni kinafaa kwa matumizi ya chakula, na kukidhi mahitaji ya mwili wa mwanadamu. Mfano, takwimu zinaonesha kuwa kiwango kikubwa cha matumizi ya soda huchangia 22% ya ugonjwa wa kisukari. Chakula bora ni kile kinachodumisha afya ya mwili na kumkinga dhidi ya magonjwa. Chakula kinatakiwa
kitumiwe katika kiwango sahihi, kulingana na uhitaji wa mtu( kazi, umri, hali ya hewa, uzito, muda, hali ya kiafya ya mtu kwa ujumla). Waeskimo wanaopatikana Alaska hutumia samaki katika kipindi kirefu cha maisha yao, lakini mara nyingi hukumbwa na madhara yanayotokana na ukosefu wa matunda pamoja na mboga mboga. Kufikia mwaka 2013 taarifa kutoka katika shirika la chakula duniani yaani FAO, ilionekana kuwa takribani asilimia 70 ya magonjwa yanayotokea katika miongo.
kadhaa ya hivi karibuni, yametokana hasa na matumizi ya wanyama kama sehemu ya mlo, pamoja na mwingiliano wa magonjwa ya binadamu pamoja na magonjwa ya wanyama.
Matumizi ya vyakula vilivyosindikwa viwandani hasa vile vyenye sukari nyingi, rangi, mafuta mengi, pamoja na kemikali mbalimbali kwa ajili ya kuongeza ladha au kuvihifadhi vidumu kwa muda mrefu, vinapendwa sana na wengi na vinazidi
kuongezeka siku kwa siku, na hivyo inaonekana ni vigumu kuepuka matumizi yake, lakini si rafiki kwa afya.
Ukweli usiopingika ni kuwa, vyakula vinavyotokana na nafaka halisi, jamii ya mikunde, matunda, na mboga za majani ni vyakula bora miongoni mwa makundi mbalimbali ya vyakula, sababu zifuatazo:
a. Huwa na virutubisho vyote vinavyopatikana kwenye vyakula vingine kama nyama.
b. Huwa na sifa ya uponyaji, kwa kuwa vina antioksidanti au viondoa sumu kwa baadhi ya vitamini pamoja na madini.
c. Ni vyakula ambavyo havina madhara vikitumiwa katika ubora wake. Lakini zaidi ni kwamba hupatikana kwa urahisi.
Kwa miaka miaka mingi vyakula hivi vimechukuliwa kama vyakula vya watu duni, lakini badala yake vimekuwa na manufaa mengi, ambayo hudhibiti gharama kwa ajili ya matibabu yanayotokana na athari za upungufu wa vyakula hivi.
Kwa karne nyingi zilizopita chakula kama kabeji imekuwa ikitumika kama kinga dhidi ya saratani, ikiwemo pamoja na uvimbe wa saratani. Wagiriki waliipenda pamoja watu walioishi zama za utawala wa warumi kama akina Hipokreti, Galemi pamoja na Diopokrati.
waliithamini kwa kuwa iliwasaidia warumi kukaa kipindi kirefu bila ya kutumia dawa.
Ikiwa unapenda vyakula vitamu kama peremende, chokoleti, sukari, keki pamoja na soda ambavyo vingekuletea madhara mbalimbali kama ongezeko la uzito, ongezeko la sukari mwilini, shinikizo la juu la damu, matatizo ya kusahau, wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo, badala yake unaweza kutumia vyakula kama asali mbichi, ndizi, viazi vitamu, mchanganyiko wa juisi mbali mbali kutoka kwenye matunda na mboga za majani kama brokoli, spinachi, karoti, nanasi, tikitimaji, zabibu, embe, tende, miwa, humpa mtu ladha maridhawa pamoja na afya mathubuti.
Tunda aina ya tofaa(Apple) hujulikana kama malkia wa matunda kwa kuwa ni tunda tamu na lenye faida nyingi ndani ya mwili kama vile, kudhibiti tatizo la kukosa choo, shinikizo la juu la damu, saratani ya utumbo mpana, sukari yake pia huwafaa hata wenye tatizo la kisukari.
1. Mazoezi na shughuli za mwili
Gari huwa haliwekewi mafuta ili liendele tu kukaa kituoni, bali limpeleke
anaeliendelesha pale anapohitaji kufika. Vile vile mwili wa binadamu hauwezi tu
kulishwa chakula na kukaa bila ya kufanya chochote, badala yake chakula hicho kinaweza kugeuka sumu, hasa kisipotumiwa pasipo utaratibu maalumu. Kukaa siku saba bila ya kufanya mazoezi huufanya mwili kuwa dhaifu.
Tafiti zinaonyesha kuwa, mlo kamili pamoja na mazoezi hupunguza uwezekano wa kupata saratani kwa 30%. Asilimia kubwa ya vijana kwa wazee hawajihusishi na shughuli za mazoezi badala yake muda mwingi hutumika kwenye runinga, mitandao ya kijamii pamoja na kazi za kukaa kama zile za maofisini. Mazoezi humkinga mtu na uzito kupita kiasi, matatizo ya moyo, huboresha mfumo wa uzazi pamoja na kuweka vichocheo vya mwili yaani homoni katika uwiano mzuri, mazoezi huboresha mzunguko wa usingizi, mazoezi huongeza homoni za furaha kama vile dopamaini na noradrenalini, zinazosaidia kuondokana na msongo wa mawazo, wasiwasi pamoja na sononeko.
3. Mahusiano mazuri ya jamii.
za kimaisha kama uchumi na mahusiano. Hali hii husababisha kinga za mwili kushuka, kukosa hamu ya kula, kukosa usingizi, upungufu wa nguvu za kiume, kutojihusisha na shughuli za mwili pamoja na mazoezi, na hivyo kumfanya mtu kupata magonjwa na maambukizi kwa urahisi.
4. Kiasi
Kila kitu kinatakiwa kifanyike au kutumiwa kwa kiasi hata kama ni kizuri ndani ya mwili, mwili ulitengenezwa.
kwa mifumo inayofanya kazi kwa utaratibu maalumu, mahitaji ya mwili yanapopungua au kuzidi, mwili huwa haufanyi kazi kama inavyotakiwa, mazoezi yafanyike kwa kiasi kulingana na mahitaji au hali ya mtu, kadhalika vilevile kwa chakula, hewa safi, muda wa kulala, muda wa kufanya kazi, muda wa kupumzika, vyote vinatakiwa vizingatiwe katika utaratibu wake.
Vile vile zipo njia zingine kadha wa kadha, zitakazoweza kusaidia kupunguza idadi ya wagonjwa pamoja na maambukizi ya magonjwa katika karne yetu, kama vile kudumisha usafi na utunzaji wa mazingira, kuwa na sera nzuri kuhusu afya na inayotekelezwa na watu wote, elimu ya afya kwa jamii kusisitizwa kupitia vyombo vya habari kama vile runinga, redio, magazeti, majarida pamoja na mitandao ya kijamii, matumizi ya maji safi na salama, kujihusisha na shughuli za ibada kama vile kuimba na kuabudu. Kutembelea vituo vya afya kwa ajili ya kupima maendeleo ya afya ya mwili kama vile shinikizo la damu, kiwango cha sukari mwilini, kiwango cha oksijeni mwilini, pamoja uwezekano wa maambukizi ya magonjwa yanayoweza kutokana na virusi, bakteria pamoja na fangasi, kwa ajili ya kuchukua tahadhari, ushauri nasaha. Salia na afya njema.
Attachments
Upvote
225