Heri ununue nyavu kuliko bodaboda

Heri ununue nyavu kuliko bodaboda

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Nyavu ya inch 3 au 5 ukiinunua mpya ni kama million 1 hivi ambayo maliasili hawatakusumbua, chombo ni ngalawa ambayo ni kama laki 2. Ukimpata baharia mzuri akasimamia na wavuvi wake 10 kazi ikafanyika una asilimia 25 ya mauzo. Mfano imepatikana 100000 basi yako ni 25000 ➕ samaki wa mboga na ikitokea wamebahatika kambakochi jua kilo 1 ni 85000.

Sasa ukijichanganya sijui bodaboda wanazingua kazi yenyewe kwa siku wanakuletea 6000 kwa utata mara boda imeharibika sijui services halafu boda umeichukua kwa zaidi ya million 3 na point.

Thread ni maalum kwa wana jamiiforums wa Mwanza, Musoma, Kagera, Kigoma, Tanga, Zanzibar, Dar, Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma.
 
Mambo yenye tija kama haya hayapo katika mitaala yetu ya elimu, tunaishia kufundishwa kilimo cha ndizi jamaica, kilimo cha chai srilanka, kilimo cha kahawa brazili aina za kawaha sijui arabika na robusta......hatufundishwi Mambo ya msingi yanayohusiana na rasilimali za nchi yetu pamoja na uhalisia wa maisha yetu. Pamoja na nchi hii kuwa na madini mengi ya aina tofauti, wananchi wake wengi hawajui chochote kuhusiana na hayo madini.
 
Kama unajitafuta wekeza kwenye kazi ambayo wewe ndo unaifanya sio mwingine anafanya halafu akipata mgawane sababu umempa vitendea kazi. Ila kama tayari umeshajipata unaweza kuwekeza kwa mtindo huu. Masikini kuutaka utajiri kupitia masikini wenzake mtaishia kutapeliana au kugombana.
 
Back
Top Bottom