Heri ununue nyavu kuliko bodaboda

Umeongea point sana mkuu.. Tukitumia rasilimali zetu vzr maendeleo yatakuja maana wavuvi wapo na wana moyo wa kazi ila vifaa tu ndo changamoto
 
Changamoto ya kwanza ni huyo baharia utakayempa hiyo nyavu.

Watanzania ni watu wa ovyo mno kwenye uaminifu hasa biashara za aina hii.
 
Huwa najaribu sana kutafakari lakini nashindwa kuhalalisha kwenye kichwa changu kumnunulia mtu bodaboda halafu kila siku au wiki aniletee pesa then baada ya muda iwe mali yake.

Yani sioni mantiki ya kutumia pesa yangu kwa mkupuo ili tu nije kupewa kidogo kidogo.
 
Labda awe ndugu yako ukaamua tu kumsaidia
 
-heri ununue kiwanja kuliko kunywa bia
-heri ukae kwako madirisha wazi kuliko kupanga
-heri uloge kuliko kwenda polisi
-heri uoe kuliko kua bachela
-heri ujenge kuliko kununua gari
-heri ujiajiri kuliko kuajiriwa
-heri ukae kijijini kuliko mjini

maficho ya bwana heri tufanye kazi kwa bidii na tutumia chansi vizuri kama wafanyavyo wanasiasa
habari za jua na mvua bora nini tuachane nazo
 
Noted
 
Rahisi tu..?? Uingie baharini ama ziwani upate samaki..???
 
Una maana ya KOKOLO au NYAVU km ulivyoiita?
 
Labda awe ndugu yako ukaamua tu kumsaidia
Labda iwe ndugu kama unavyosema. Lakini utakuta vijana wanafosi uwanunulie bodaboda ya mkataba kama vile kuna faida kubwa sana mimi mnunuzi napata.

Nahisi ina mantiki kwa wale wenye uwezo wa kununua nyingi. Lakini mimi nitoe 2.8 yangu halafu recovery yake iwe kwa mahesabu ya elfu kumi kumi tena ya kutafutana, sioni mantiki yake.
 
Hizi ni Biasgara za watu ambao kichwani hakuna, ni ujinga sana, ni zaidi ya ujinga, eti pikipiki ya mkataba, full ujinga
 
Mkuu ungekuwa na picha ya hizo nyavu ingependeza zaidi.Niko pande hizi za mother city nyavu zinapatikana sema ujuzi wa kuzitambua ndiyo tatizo.Niko interested na ajira za kwenye maji.Kila kitu cha uvuvi na majini kinapatikana pande hizi.
 
Mkuu ndo maana nimekwambia upate muaminifu ila pia ukiamua kwenda kila siku wanapofanya mnada unaweza kucheza nao
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu samaki huwa zinahamishiwa hata kwa wavuvi wengine majini na kuna wachuuzi wanafwata mzigo majini afu wakitoka forodhan unazan siku haikuwa nzuri kumbe washajiongeza,nilipata hii experiance ziwa rukwa upande wa chunya
 
Hv
Hivi unajua wizi wa nyavu ulivyoshamiri?? Kuna mtu aliniambia ziwa viktoria maeneo ya Ukerewe ukinunua nyavu ukakaa nayo wiki 2 basi mshukuru sana Mungu. Sipingani na hoja zako but angalia na negative pia za nyavu kuliko ulivyolalia negative za boda
 
Ulisemalo ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…