Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½Eid Mubarak πβ¨
View attachment 3560106
Nawatakia nyote sikukuu njema iliyojaa furaha, amani na baraka tele.
Mwenyezi Mungu azikubali ibada zenu zote, awajaalie afya njema na mafanikio katika kila jambo mlipangalo.
Tukumbuke kushirikiana na kusaidiana, hasa wale wenye uhitaji, ili furaha ya Eid iwafikie wote π€
Eid hii iwe mwanzo wa neema mpya, upendo zaidi na mshikamano katika jamii zetu.
NdioNaomba niulize tu, Kesho Eid?
Mwezi umeonekana Kenya.Sawa sawa mkuu...nilikuwa naangaza angaza kuona kama kuna habari yoyote mitandaoni kutoka mamlaka zetu, naona bado wako kimya.
Nazungumzia Tz mkuu.
Duh.....Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema mwezi haukuandama hivyo Eid al-Fitr ni Machi 21, 2026.
View attachment 3560150
Wenye mamlaka wamegoma.....Mwezi umeonekana Kenya.
Hivyo eid tunasherehekea.
Kiongozi Kwa mujibu wa Sheria ipi ya kiislam?Kiongozi wenu kasema 30 ni jmosi mwezi haujaatoka.
Nyie walafi kesho mnafungua,ina maana hata hatuelewani huko.
Nyie hata mwaka ujao mle Eid hakuna anayejali.
Komaeni tu
Ni utaratibu kuwa na viongozi katika dini nyingi hapa duniani.Mufti ni nani katika Uislamu? Waislamu wanafunga na kufungua Kwa mujibu wa mwezi au mufti?
Bakwata unamfahamu.Kiongozi Kwa mujibu wa Sheria ipi ya kiislam?
Sawa mgalatia.Bakwata unamfahamu.
Mle leo au kesho hata keshokutwa kwangu mgalatia ni siku ya kawaida tu.
Labda dini nyingine, lakini Waislamu hufuata Sheria na sio kauli za watu hasa wale ambao vyeo vyao havitambuliki katika kitabu chaoNi utaratibu kuwa na viongozi katika dini nyingi hapa duniani.
Waislamu wa Tanzania wanasubiria Eid ya maelekezo kutoka Magogoni. Nasikia mgeni rasmi wa Eid ni mwenye nchi lakini kwa bahati mbaya hali yake sio nzuri kwahiyo tusubrie hadi jumamos hali yake itakuwa sawa tusherekee Eid ya maelekezo.