Heri ya siku ya kuzaliwa kwako Rais Mstaafu Mzee Jakaya Mrisho Kikwete

Heri ya siku ya kuzaliwa kwako Rais Mstaafu Mzee Jakaya Mrisho Kikwete

%E2%9C%8C%EF%B8%8F%E2%9C%8C%EF%B8%8F%E2%9C%8C%EF%B8%8F.jpg

Leo ni siku yake ya Kuzaliwa , ambapo Taarifa zinaonyesha kwamba alizaliwa tarehe 7/10/1950 .

Binafsi namtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa , Pia naomba ku DEDICATE ujumbe huu muruwa alioutoa kwenye Mkutano Mkuu wa ccm mwaka 2012 , ambapo aliwaomba wanaccm kujibu hoja za Wapinzani kwa ufasaha BADALA YA KUKASIMISHA MAMLAKA YA CHAMA CHAO KWA JESHI LA POLISI

FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Sasa hapa "dada mkubwa" tujadili tarehe ya kuzaliwa au tujadili nukuu za CCM?
 
Jamaa sijui siku hizi anajisikiaje akimuona Mkwere maana si kwa mkwara ule.

"Wastaafu Hawa wakae Kimya"
Screenshot_20211007-134832.jpg
 
Msowger king

Bila huyu mzee ningesugua soli Sana kitaa hadi ningekomaa

Nashukuru nilimaza chuo kabla ya lile jiwe jeusi halijaja kwenye hatamu ,to hell with him[emoji849]
 
View attachment 1966688

Leo ni siku yake ya Kuzaliwa , ambapo Taarifa zinaonyesha kwamba alizaliwa tarehe 7/10/1950 .

Binafsi namtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa , Pia naomba ku DEDICATE ujumbe huu muruwa alioutoa kwenye Mkutano Mkuu wa ccm mwaka 2012 , ambapo aliwaomba wanaccm kujibu hoja za Wapinzani kwa ufasaha BADALA YA KUKASIMISHA MAMLAKA YA CHAMA CHAO KWA JESHI LA POLISI

View attachment 1966687
Ndio maana Mimi naamini katika hii nchi kuna magwiji watatu tu wa siasa za hii nchi

J.K nyerere

J.m kikwete

Na Mwamba F.A mbowe

Wengine wote hawaijui siasa wanaifanya kwa kubahatisha tu.

Hawana misimamo vigeugeu

Hawana teknik wako wako sio lowassa ,sio slaa ,sio zitto sio Nani

Hao watu watu watatu unaweza ukawaandikia kitabu chenye madini sana kuhusu siasa zetu hizi

Hao ndio majabali ninaowakubali

Usijesema nimemsahau lissu

Lissu kwangu ni mchanganyiko wa siasa na harakati

Yuko vizuri sana kwenye harakati kuliko siasa japo havipishani sana

Wengine wote wanatembelea nyota na mbeleko za washua zao,anko zao,madanga yao,ving'asti wao
 
kikwete-pic-data.jpg

Ni tarehe 07.10.1950 ndiyo siku ambayo Mzee Jakaya Kikwete alizaliwa!

Mzee Kikwete ukiwana kama binadamu kama wengine huwezi kosa mapungufu,lakini Mimi hua nasema wewe ni mmoja wa wanasiasa waliokomaa!

Kipindi cha uongozi wako, kulikuwa na uhuru sana, tofauti kabisa na awamu ya tano, watu walikua wanapata ajira,pesa zilikuwepo na walikua wanaendesha maisha yao vizuri tu!

Nakutakia maisha marefu na yenye baraka tele, uweze kugonga hadi miaka 95 huko kama kina Mzee Madiba Nelson Mandela
Hbd
 
JK the legend, uishi miaka mingi we mzee.
 
Haweki vitu moyoni hata siku moja. Ndio maana anaishi maisha marefu akiwaacha wengi wakifa siku sio zao kwa kutunza hasira na mavinyongo mengi tu ndani ya nafsi zao.​

Hakuna mwenye akili na hekima, awe CCM au vyama vya upinzani, awe mkristo, muislam au asiye na dini, asiyempenda Kikwete.

Jakaya Kikwete, unapendwa kwa utu wako, hekima yako na uvumilivu wako.

Kwa hayo mema kwa wanadamu wenzako, Mungu wa rehema akuzidishue maisha yenye heri.
 
JK aliwapiga virungu watu ila hakuna anaemchukia

Sasa kuna walio sasa wanadhani ukipiga virungu ndio utapendwa na watu .

Wakaksi kila Kona ukipingana msimamo na serikali watakusaka hadi uvunguni Wana roho za kishweitan wamerithi kwa yule "aliyeenda zake"

Acha hizo huo sio utanzania

Wala sio uzalendo ni uzandiki tu
 
Msowger king

Bila huyu mzee ningesugua soli Sana kitaa hadi ningekomaa

Nashukuru nilimaza chuo kabla ya lile jiwe jeusi halijaja kwenye hatamu ,to hell with him[emoji849]

Hongera sana mkuu, wengine tunaendelea kuugulia maumivu ya mwendazake hadi kwenye awamu hii
 
Happy Birthday Honorable JAKAYA MRISHO KIKWETE.
 
Back
Top Bottom