Heri ya siku ya kuzaliwa kwako Rais Mstaafu Mzee Jakaya Mrisho Kikwete



Leo ni siku yake ya Kuzaliwa , ambapo Taarifa zinaonyesha kwamba alizaliwa tarehe 7/10/1950 .

Binafsi namtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa , Pia naomba ku DEDICATE ujumbe huu muruwa alioutoa kwenye Mkutano Mkuu wa ccm mwaka 2012 , ambapo aliwaomba wanaccm kujibu hoja za Wapinzani kwa ufasaha BADALA YA KUKASIMISHA MAMLAKA YA CHAMA CHAO KWA JESHI LA POLISI

 
Sasa hapa "dada mkubwa" tujadili tarehe ya kuzaliwa au tujadili nukuu za CCM?
 
Jamaa sijui siku hizi anajisikiaje akimuona Mkwere maana si kwa mkwara ule.


"Wastaafu Hawa wakae Kimya"
 
Msowger king

Bila huyu mzee ningesugua soli Sana kitaa hadi ningekomaa

Nashukuru nilimaza chuo kabla ya lile jiwe jeusi halijaja kwenye hatamu ,to hell with him[emoji849]
 
Ndio maana Mimi naamini katika hii nchi kuna magwiji watatu tu wa siasa za hii nchi

J.K nyerere

J.m kikwete

Na Mwamba F.A mbowe

Wengine wote hawaijui siasa wanaifanya kwa kubahatisha tu.

Hawana misimamo vigeugeu

Hawana teknik wako wako sio lowassa ,sio slaa ,sio zitto sio Nani

Hao watu watu watatu unaweza ukawaandikia kitabu chenye madini sana kuhusu siasa zetu hizi

Hao ndio majabali ninaowakubali

Usijesema nimemsahau lissu

Lissu kwangu ni mchanganyiko wa siasa na harakati

Yuko vizuri sana kwenye harakati kuliko siasa japo havipishani sana

Wengine wote wanatembelea nyota na mbeleko za washua zao,anko zao,madanga yao,ving'asti wao
 
Hbd
 
JK the legend, uishi miaka mingi we mzee.
 

Haweki vitu moyoni hata siku moja. Ndio maana anaishi maisha marefu akiwaacha wengi wakifa siku sio zao kwa kutunza hasira na mavinyongo mengi tu ndani ya nafsi zao.​

 
Hakuna mwenye akili na hekima, awe CCM au vyama vya upinzani, awe mkristo, muislam au asiye na dini, asiyempenda Kikwete.

Jakaya Kikwete, unapendwa kwa utu wako, hekima yako na uvumilivu wako.

Kwa hayo mema kwa wanadamu wenzako, Mungu wa rehema akuzidishue maisha yenye heri.
 
JK aliwapiga virungu watu ila hakuna anaemchukia

Sasa kuna walio sasa wanadhani ukipiga virungu ndio utapendwa na watu .

Wakaksi kila Kona ukipingana msimamo na serikali watakusaka hadi uvunguni Wana roho za kishweitan wamerithi kwa yule "aliyeenda zake"

Acha hizo huo sio utanzania

Wala sio uzalendo ni uzandiki tu
 
Msowger king

Bila huyu mzee ningesugua soli Sana kitaa hadi ningekomaa

Nashukuru nilimaza chuo kabla ya lile jiwe jeusi halijaja kwenye hatamu ,to hell with him[emoji849]

Hongera sana mkuu, wengine tunaendelea kuugulia maumivu ya mwendazake hadi kwenye awamu hii
 
Happy Birthday Honorable JAKAYA MRISHO KIKWETE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…