Tunapoadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika na baadae Tanzania, tujikumbushe maneno ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuhusu Muungano wa Tanzania.
Watanganyika mpaka muda huu tuko nyuma kwa goli 3 kwa bila dhidi ya Wazanzibari! Halafu ndiyo kwanza tuko dakika ya pili tu ya mchezo! Mpaka zitakapo malizika dakika zote 90, huenda tukafungwa hata magoli 100 na hawa jamaa zetu wasio na visogo.