Mfahamu mwanamitindo maarafu wa kiwango cha kimataifa Herieth Paul, ambaye ni raia wa Tanzania aneyeishi nchini Canada. Mwanamitindo huyu mwenye umri wa miaka 18 anafanya shughuli zake jijini New York Marekani, London Uingereza na Milan Italia. Amesaini mkataba wa vipodozi na kampuni maarufu duniani ya Calvin Klein na ametokea katika kurasa mbele za majarida mashuhuri mbalimbali kama Elle Magazine, Teen Vogue na VogueItalia. Hivi karibuni pia mrembo huyu amekuwa miongoni mwa wanamitindo watatu waliochaguliwa katika kampeni ya kutangaza mavazi ya msimu wa spring ya mbunifu maarufu wa mavazi duniani, Tom Ford.