Heritage financing company limited inavyouza mali za watu walioshindwa kurudisha fedha za mikopo

Heritage financing company limited inavyouza mali za watu walioshindwa kurudisha fedha za mikopo

Kibogoyio2020

Senior Member
Joined
May 4, 2018
Posts
154
Reaction score
77
Jf. Kampuni ya heritage financing company limited iliyoko Arusha mjini inyokopesha mikopo kwa riba ya 100% imeendeleza kilio nchini kwa kuuza nyumba za watanzania bila kufuata taratibu wala sheria za nchi yetu. Kila kona wananchi wanalizwa. Ukifika mahakama yeyote hapa Arusha utakuta kesi zaidi ya kumi ya hii kampuni. Waliowahi kuuziwa nyumba ,magari, viwanja, no kampuni hii. Tukutane hapa
 
Jamani! Kama mtu huna sababu ya msingi ya kuchukua mkopo usikope! Ukikopa ukaweka dhamana nyumba, basi wakati unasaini mkopo ujue kabisa hiyo nyumba ushaiuza na chance za kuiokoa ni 20%!
Unapokula pesa za mkopo ujue kabisa kinachoweza kukupata. Ni hayo tu.
 
Duh! Riba 100%!
Bot tunashauri hii kampuni ichunguzwe. Hawa ni wapiga dili muda mrefu. Uchunguzi uanzie miaka mitano kurudi nyuma.unakopeshwa 10.000.000 Kwa miezi sita kila mwezi unalipa 1.000.000 na baada ya miezi sita unawarudishia 10.000.000 kwa maana hiyo unakuwa umewalipa 6.000.000+10.000.00=16.000.000 Mimi sijasoma hesabu hapa riba ni kiasi gani? Bado wanakukata% ya kushughulikia mkopo pamoja na application fee. Hapa monduli wameuza nyumba jana
 
Yaani hawa wanaaply bullet payment kwa mkopo mduchu tena wa muda mfupi,wamulikwe aina ya ulipaji wao inatakiwa uwe kwenye big and long term invenstment Kibogoyio2020,
 
Jf. Kampuni ya heritage financing company limited iliyoko Arusha mjini inyokopesha mikopo kwa riba ya 100% imeendeleza kilio nchini kwa kuuza nyumba za watanzania bila kufuata taratibu wala sheria za nchi yetu. Kila kona wananchi wanalizwa. Ukifika mahakama yeyote hapa Arusha utakuta kesi zaidi ya kumi ya hii kampuni. Waliowahi kuuziwa nyumba ,magari, viwanja, no kampuni hii. Tukutane hapa
SASA MNAKOPA ZA NINI ?
nimepekua na kuwapata riba yao kwa mikopo ya dharura kweli ni juu km 60% na sio 100%
143653722132786.jpg

kwa ushauri km huna biashara usikope kabisa kwa kuweka dhamana nyumba
kiMahakama nyumba haiuzwi mpaka wakutangazie siku 74 miezi miwili na nusu na tena kwa kubandika Tangazo kwenye nyumba yako
Nahata kabla ya Dalali unaombwa wewe mwenyewe umtafute Dalali
kwa kipindi hico ukilipa Kesi inahama tena (kwanini usiiuze mwenyewe)
haya makampuni ya Financial intity yameruhusiwa kisheria kwa hiyo yaepukeni
 
Jamani heritage financing company limited iliyoko hapa Arusha Tanzania ni shida. Wanapenda riba kubwa, wanapenda kuuza mali za watu,wanapenda makesi mahakamani la kushangaza kupita kiasi mkurugenzi wa kampuni hii ni mlokole. ova
 
nyumba inauzwa kwa amri ya mahakama, mahakama zetu huwa zinabariki mikataba hii haramu kwa nini?Nilisoma mahala ili mkataba uwe na nguvu ni lazima uwe halali. Riba 100% bot na tra wanajua hii!
Kwa upande wa kuthibiti riba serikali labda kwa makusudi au la imelizembea sana. Riba ya 100% ni mauaji ya halaiki na kuna vikampuni vingi tu mitaani vinatapeli na serikali ipo tu.
 
Kibogoyio2020,

HAWA NI WAUWAJI KABISA, KUNA JAMAA YANGU ANAKAA ARUSHA WAMEMMALIZA, HAWANA UTU KABISA, ILA WAMESAHAU, NA TAMAA YAO HAITAWASAIDIA, WATU WOTE WA MIKOPO KWA NAMNA YA DHULUMA WAMEISHIAGA KWENYE BALAA NA VIFO VIBAYA
 
Jamani heritage financing company limited iliyoko hapa Arusha Tanzania ni shida. Wanapenda riba kubwa, wanapenda kuuza mali za watu,wanapenda makesi mahakamani la kushangaza kupita kiasi mkurugenzi wa kampuni hii ni mlokole. ova

WEZI
 
kama ndo hvi itafungwa kwakukosa wateja maana wamejiharbia soko
 
Kibogoyio2020, Wakati mnakopa mlisoma maelekezo ya mkopo ?

Je mliwauliza bot kuhusu uhalali hilo swala?
Je kuna mahali wamewadanya au ?

Hii ni hatari sana kwa taifa kama sehemu wanayojiite ni wasomi toka enzi za mkoloni wanalilia kwamba wametapeliwa je sehemu nyingine itakuwaje?
 
Konsciouz, mikataba inayokubalika kisheria ni ile iliyoko kwenye sheria za nchi, huu ni sawa na kukibaliana kwenda kuua halafu ukimbilie mahakamani, wanasheria hebu njooni mtutafsirie
 
utakuta mkataba wa milioni kumi unajumlishwa na hiyo riba 6m mkataba unasoma umekopeshwa 16m unasainiwa hakimu akijua kinachoendelea, tena wana mahakimu wao kule wilayani,wakikatiwa laki 5 hazina risiti, wanagonga na mihuri ua jamhuri kabisa, wanajitia wanatoa huduma, hii si sawa (kwa sauti ya Nape)
 
Back
Top Bottom