Hersi akiri Yanga imekiuka mkataba na SportPesa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Wakati mazungumzo yakiendelea kuhusiana na hatma ya mkataba kati ya Yanga na mdhamini wao SportPesa, Rais wa Yanga Hersi Said amekiri kuwa baadhi ya vipengele vilivyokuwa vinaibana Yanga wamevikiuka katika mkataba wake na SportPesa.

Akihojiwa na kituo cha Television cha Clouds, Hersi amesema kuwa baada ya kuingia mkataba mpya na kampuni ya Haier, baadhi ya vipengele ambavyo Yanga wanatakiwa kuendelea kuvitekeleza ni pamoja na kuvaa kits za SportPesa katika mazoezi au wakati wanasafiri, kuiweka logo ya SportPesa katika banners wakati wa press conference na katika mawasiliano ya social media.

Kusikiliza kipande hicho angalia video hii kuanzia 12:10-

Hata hivyo ushahidi upo unaoonyesha kuwa toka waingie mkataba na kampuni ya Haier, Yanga wamekuwa hawatimizi mahitaji hayo ya mkataba.

20230302_120929.jpg
20230302_121204.jpg

20230302_122345.jpg
 
Na bado kuna wavimba macho walikuwa wanatetea huo ujinga wa kushabikia ukiukaji wa mkataba.Mkataba ni jambo la kisheria haupingwi kwa ushabiki kwani ukweli huwa unadhihiri na hapo uongo unajitenga
 
Baada ya kuiangalia hiyo clip nimeamini Yanga walifanya chaguo sahihi kabisaa (Eng. Hersi) japo kuna kaufala ka kujisahaulisha contents ndogondogo
 
Sasa watalipa gharama za fidia? Au labda sportpesa hawana shida na huo uvunjaji wa mkataba.
Ni kweli kabisa, wamewafanyia uhuni sana SportPesa.

Ningewaelewa sana Yanga kama wangezalisha jezi za kuvaa wachezaji tu, wakati wa hizo mechi za makundi. Na sio kutengeneza jezi za kuvaa mashabiki. Maana yake ni kuwa mashabiki wataendelea kuvaa jezi za Haier hata katika mechi za ligi kuu na kuwanyima SportPesa haki yao ya kutangazika.

Ila kingine naona SportPesa kwa kuwa hawana klabu nyingine kubwa inayoweza kuwapa promotion nje ya Yanga, ndio maana wameogopa kuvunja mkataba, wamekubali kufa kikondoo.
 
Hilo suala la jezi nimekuwa naliwaza pia na mimi. Ni kweli kabisa wangetengeneza jezi za wachezaji na benchi la ufundi pekee bila za washabiki hili jambo lingekuwa dogo zaidi. Ila pia kwa upande mwingine wangefanya hivyo ingeonekana kama wanajishtukia wakaamua kujilipua.
 
At least hoja yao ya "kifuani pasikae wazi" ingeweza kuwa na mashiko, kwani mashabiki bado wangeendelea kuvaa za SportPesa.
 
Ni kweli kabisa, wamewafanyia uhuni sana SportPesa.

Ningewaelewa sana Yanga kama wangezalisha jezi za kuvaa wachezaji tu, wakati wa hizo mechi za makundi. Na sio kutengeneza jezi za kuvaa mashabiki. Maana yake ni kuwa mashabiki wataendelea kuvaa jezi za Haier hata katika mechi za ligi kuu na kuwanyima SportPesa haki yao ya kutangazika.

Ila kingine naona SportPesa kwa kuwa hawana klabu nyingine kubwa inayoweza kuwapa promotion nje ya Yanga, ndio maana wameogopa kuvunja mkataba, wamekubali kufa kikondoo.
Too bad kwa sportpesa.
 
Mwanzo alikuwa mtata anabisha hadi mishipa ya shingo inamtoka

Leo anakuja kusema amekiuka

At least kawa muungwana
Madunduka ni wagumu kuelewa,rage alikua sahihi,kasema wamekiuka Kwa kutovaa nembo sportpesa wakiwa safarini na mazoezini siyo Ile mbele ya shati
 
Back
Top Bottom