Hesabu ni somo rahisi kuliko chochote! Tusiliogope!

Hesabu ni somo rahisi kuliko chochote! Tusiliogope!

Kutoka Mirembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
294
Reaction score
87
Hello waungwana!
Imekuwa ikisemekana kuwa hesabu na masomo ya Sayansi ni ngumu sana na ugonjwa wa taifa!
Lakini kwa uzoefu wangu,nimegundua shida kubwa ipo katika mtazamo tunao jengewa na kujijengea toka ngazi ya awali kabisa.

Sifa kubwa ya hesabu ni kutegemeana kwa topic toka darasa la kwanza hadi University!
Hivyo,kuna umuhimu wa kuwajengea watoto wetu mapenzi na hesabu toka wakiwa darasa la kwanza.

Kwa mliopo ngazi za juu,na unaona hesabu kama janga kubwa,hamjachelewa bado!
Shida kubwa ipo kwenye mtazamo.
Jaribu kuilazimisha akili yako kuwa hesabu si kitu cha ajabu,halafu anza kujifunza basics zake taratibu.

WIMBO
Hesabu,ni nzuri sana wee,
hesabuu,ni nzuri sana wee..
We mwalimu we mwalimu nifundishe.X2
Ukisha nifundisha,siwezi kusahau,
ee mwalimu,ee mwalimu nifundishee.

Kutoka Mirembe.
 
Last edited by a moderator:
Hesabu kama ni rahisi hivyo mpaka mtu wa Milembe anazijua basi hakuna sababu yoyote ya msingi watoto wetu kufeli
 
Nilivyoiona title ! Nikajua alieandika analiogopa sana !

Lakini La hasha !
 
Nilivyoiona title ! Nikajua alieandika analiogopa sana !

Lakini La hasha !

Mkuu snipa,
Hakuna kitu rahisi kama vitu objective,
kuna kanuni tayari ambazo ukizifuata unafikia hitimisho lile lile.
Infact ni rahisi kupata 100% ya Maths na Physics,kuliko Kiswahili au History.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu snipa,
Hakuna kitu rahisi kama vitu objective,
kuna kanuni tayari ambazo ukizifuata unafikia hitimisho lile lile.
Infact ni rahisi kupata 100% ya Maths na Physics,kuliko Kiswahili au History.

Simu !

Mapenzi !

Uhuni & Utozi !

Starehe !

Dharau !

Kiburi & Jeuri !

Wazazi !

Ukiniambia mimi nitoe sababu za watoto kufeli ! Nitasema hizo hapo ! Wala sitamtaja MWALIMU !
 
Last edited by a moderator:
ukiwa na bidii lazima utapata A ya hesabu, ni somo lililo direct sana halina longolongo, ni rahisi kupata A ya hesabu kuliko somo lolote lile kwani halitegemei amesahihisha nani
i love mathematics
 
ukiwa na bidii lazima utapata A ya hesabu, ni somo lililo direct sana halina longolongo, ni rahisi kupata A ya hesabu kuliko somo lolote lile kwani halitegemei amesahihisha nani
i love mathematics

Me too. I love mathematics
 
Me either I lov mathmatcx

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
nakubaliana na wewe lakini mkuu kubali kataa kuna baadhi ya topic baba ni balaaaa......
Nitakupa chache tu nyingine wadau watasema wenyewe
Topic za o level
CIRCLE AND SPHERE (FORM THREE)
TRANSFORMATION (FORM FOUR)
TRIGONOMETRIC RATIO haswa kwenye application yake ya angle of elevation and depression (FORM TWO)
Topic za A level
Binomial theory (FORM FIVE)
INTEGRATION AND DIFFERENTIAL haswa kwenye trigonometrical ratio na graph zake
NITARUDI BAADAE
 
ukiwa na bidii lazima utapata A ya hesabu, ni somo lililo direct sana halina longolongo, ni rahisi kupata A ya hesabu kuliko somo lolote lile kwani halitegemei amesahihisha nani
i love mathematics

Mkuu Naipenda Hisabati Ila Siijui Upo Tayari Kunifundisha?
 
sioni kama topic ulizozitaja ni ngumu ila ni kama mtoa mada alivyoeleza hapo mwanzo.
 
nakubaliana na wewe lakini mkuu kubali kataa kuna baadhi ya topic baba ni balaaaa......
Nitakupa chache tu nyingine wadau watasema wenyewe
Topic za o level
CIRCLE AND SPHERE (FORM THREE)
TRANSFORMATION (FORM FOUR)
TRIGONOMETRIC RATIO haswa kwenye application yake ya angle of elevation and depression (FORM TWO)
Topic za A level
Binomial theory (FORM FIVE)
INTEGRATION AND DIFFERENTIAL haswa kwenye trigonometrical ratio na graph zake
NITARUDI BAADAE

Ngoja wadau waje waseme,
ila amini nakwambia zinaonekana ngumu kwa sababu ya ku delay kwenye topic mojawapo level ya nyuma.
Mfano,Circle inategemea sana hesabu za nyuzi za drs la sita na fm one,pamoja na triangles ya fm two.
Hzo zingine,kama Trig,Binomial na Calculus vina majina ya kutisha tu,lakini ni vitu vya kawaida.
 
asiwadanganye mtu kuwa HESABU ni somo rahisi, hesabu sio rahisi kwa kuwa ni sayansi na somo lolote la sayansi ni gumu kwa sababu linahitaji udadisi sana, na unahitaji kujua vitu sana ili uweze kufaulu hesabu. lazima uwe unajua lugha vizuri ili uweze kubadili swali(problem) kwenda kwenye calculation mathematically. pia hesabu linahitaji sana uwe mdadisi kwa kiasi kikubwa vinginevyo utasema rahisi kama unajumlisha na kutoa. kuna hesabu mtu unapewa alafu unatumia hadi nusu saa kufikiria ugundue mtego. wakati masomo mengine KAMA HISTORY,CIVICS,BIOLOGY,AGRICULTURE KWA KIASI KIKUBWA YANAONGOZWA NA UWEZO WA KUKARIRI NA SI UWEZOWA KUDADISI. na ukitaka kujua angalia matokeo YA MATHEMATICS NA PHYSICS O LEVEL utaona yana ufaulu kidogo sana ukilinganisha na masomo ambayo yanaongozwa na uwezo wa kukariri na si udadisi.

WATU WENYE UBONGO WA KUDADISI NI WACHACHE SANA NA WENGI WANA UWEZO WA KUKARIRI, NDIO MAANA PHYSICS LINASOMWA NA WATU WACHACHE SANA NA KAMA HESABU IKIWAOPTIONAL NAYO ITASOMWA NA WATU WACHACHE SANA KWA KUWA WATU WENGI HUWA HAWANA UWEZO WA KUDADISI(CURIOSITY). lakini kwa wenye uwezo wa kudadisi hesabu lazima iwe nyepesi kwao na wanaona kukariri masomo kama histori ni shida kwa kuwa ktk topiki nzima mtaalamu wa hesabu anatumia uwezo kidogo sana wa kukariri kama KANUNI 4 AMA TANO TU alafu maswali atayafanya kwa udadisi wake, lakini anayesoma history atalazimika kukariri sehemu kubwa ya maelezo na udadisi unatumika kidogo sana. NA WATU WENYE UWEZO WA KUKARIRI NI WENGI.
 
Ngoja wadau waje waseme,
ila amini nakwambia zinaonekana ngumu kwa sababu ya ku delay kwenye topic mojawapo level ya nyuma.
Mfano,Circle inategemea sana hesabu za nyuzi za drs la sita na fm one,pamoja na triangles ya fm two.
Hzo zingine,kama Trig,Binomial na Calculus vina majina ya kutisha tu,lakini ni vitu vya kawaida.
CLAIMING CAPACITY IS NOT EQUAL TO CURIOSITY. hesabu si nyepesi kwa kuwa inahitaji udadisi mkubwa. nilikuwa bingwa wa topic ya circle lakini huko form one na form two sikuwa na msingi kabisa wa hizo topiki unazotaja. MASOMO YA SAYANSI HUWA WENGI WANAYAPENDA SANA FORM ONE KWA KUWA YANA VITU VINAVUTIA, FORM TWO MAMBO YAANZA KUBADILIKA PALE UNAKUTA MAMBO YA UDADISI YANAKUWA MENGI NA WENGI WANAANZA KUKATA TAMAA NA KUAMUA KUACHANA NAYO JAPO WANAYAPENDA. WENGI WA WANAFUNZI WALIOACHA KUSOMA SAYANSI UKIWAULIZA WATAKWAMBIA WALIACHANA NAYO BAADA YA KUONEKANA MAGUMU AMA KUWASHINDA, LAKINI MPAKA WANAKATA TAMAA UJUE WAMEJARIBU SANA IKASHINDIKANA
 
Hesabu ni rahisi kwa kila aaminiye kuwa hesabu ni rahisi, lakini kwa asiyeamini ni ngumu hakuna mfano, na hapo ndipo unapohitajika uvuvio wa kuwaokoa.
 
Kutoka Mirembe nakubaliana na wewe kua hisabati ni somo rahisi ktk ngazi zote ila kuna ngazi flani ina kitu kinaitwa "Abstract Algebra" kikifuatiwa na "Functional Analysis", bwana wee ukipita salama hizo sehemu basi wewe ni bingwa wa hisabati. Vinginevyo naunga mkono mada yako na ulichokisema kuhusu watu kukosa msingi mzuri ni kweli kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom