Hesabu: Tafuta umri wa sasa wa Michael

Hesabu: Tafuta umri wa sasa wa Michael

Ziltan

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
2,672
Reaction score
6,880
Umri wa Michael ni 3/5 ya umri wa mama yake. Ikiwa miaka 20 iliyopita, umri wa Michael ulikuwa 2/5 ya umri wa mama yake wakati huo. Tafuta umri wa sasa wa Michael.

Wadau karibuni tupanue mawazo.
 
SOLN
Tuseme umri wa mama ni X

MICHAEL =3/5X

Miaka 20 iliyopita

MICHAEL MAMA
3/5X-20 = 2/5(X-20)
3/5X-20=2/5X-8 ----------(Fungua mabano)
combine like terms

3/5X-2/5X=-8+20
1/5X=12
Zidisha kwa 5 kila upande
5*1/5X=12*5
X=60
Kwa hiyo umri wa mama ni miaka 60 na umri wa michael ni 3/5*60=36
Umri wa michael ni miaka 36
 
jibu ni miaka 36.
umri wa michael wa sasa ni 3/5a, "a" ukiwa umri wa mama yake wa sasa.
miaka ishirini iliyopita, umri wa michael ulikuwa 2/5 (a - 20).
sasa tuunganishe hiyo mitajo miwili kuwa mlinganyo.
3/5a - 20 = 2/5 (a-20).
3/5a - 20 = 2/5a - 40/5,
3/5a - 20 = 2/5a - 8,
3/5a - 2/5a=20-8,
1/5a=12,
5 × 1/5a=12 × 5,
a=60, hui ni umri wa mama yake michael.
kupata umri wa sasa wa michael, chukua 3/5 ya umri wa sasa wa mama yaani 60.
3/5 × 60 = 180/5 = 36.
huo ni umri wa sasa wa michael
 
Excellent bahati30 kifupi swali hili nimelitoa kwenye kitabu cha '' Msemwa, P. B. Mitihani 12 ya hisabati kwa daraa la 5; 6; na 7.
Mtihan wa 1. Yeye jibu lake ni 24 kitu ambacho si kweli,

Serikali iangalie vitabu vilivyoko sokoni.

Pw
 
Ziltan,

Mkuu vile vitabu ni majanga. Watu hawaangalii tena kusaidia kizazi kinachokuja. Wao ni mwendo wa Chapaa 2.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom