Hesabu ya maisha, vipi kwa maamuzi haya nimebugi au iko poa?

Hesabu ya maisha, vipi kwa maamuzi haya nimebugi au iko poa?

Nadhani Mkeo ndie Yuko sahihi,
1: kuhonga 7m ili uanze kulipa kodi ya 200k from 400k sio hesabu kabisa hahaha, gawanya hio 7m kwa laki 2 ambazo unaona ume save, utapata miezi 35. ukimaliza hii ndo utaweza kusema umeokoa gharama... tofauti na hapo laki 2 ulo save kodi ushaihonga.

2:kujenga ni kuzika pesa, USIKOPE KWA AJILI YA KUJENGA unless huo mkopo hauna riba. lakini still bado sio wise decision kukopa ili ukanunue tofali.

Issue nayoona hapa una ego. na hii ndo inaweza kuku cost. curb your ego, fuata ushauri wa mkeo jenga servant qrt hamia.. endelea ujenzi unaotaka polepole bila stress za kodi huku ukisimamia kinachoendelea site mwenyewe
 
Ujenzi hasa nyumba ya kwanza unahitaji umakini wa hali ya juu , kuna vitu vingi hatuvijui kuna hesabu nyingine zipo nje ya makaratasi hyo nyumba unayodhani itagharimu 90 M inaweza kwenda 150 kumbuka sasa hivi nondo na vifaa karibia vyote vya ujenzi vimepanda zaidi ya mara 2 . Yote unayoyawaza yapo sawa lakini kitendo cha kuhonga milioni 7 ili ulipe kodi laki mbili sijaelewa logic yako
 
Nina miaka 34, Mke na watoto 2,Mwaka Jana nilikua na shauku ya ujenzi kiwanja nilisha nunua kina tofali kama 4000,Kokoto mende 3, mchanga mende 3, Tank za maji lita 4000. Nikatafuta mtaalam akanichorea ramani na kunifanyia tathmini ya ujenzi ni nyumba ya vyumba 3 master moja chini na kigorofa kina chumba kimoja master.

BOQ inahitaji 10m ya msingi tu nje ya material zilizoko site. Total garama ni kama 90m ujenzi kuisha. Kodi nilikua nalipa laki 4 na nusu nyumba ya room tatu. Ambayo ilikuwa kama 30km kutoka eneo langu la ofisi. Ikizingatiwa wife ni graduate kwa sasa hana kipato.

Mafuta ya gari almost laki 2na nusu kwa mwezi. Ikabidi nifanye màamuzi nitumie kama 7m kupata nyumba ya NHC ina vyumba 2, sebule jiko na public toilet, ambayo ipo 5km kutoka ofisini kwangu, na kodi ni laki 2 ambayo nailipa kila tareh 15 ya mwezi unaofuata.

Hii nilifanya ili niweze kushusha garama zangu za maisha ili kuweza kufanikisha dream house yangu. Wife alishauri kujenga servant house tuhamie ambayo ingegharimu kama 20 - 25m na site ipo 25km kutoka ofisini wazo Lake sikulipokea nikaamua on NHC apartments. Ambayo wife hana furaha nayo.

Ila mm natazama mbali kidogo na mwaka huu 2022 nataka nichukue ka mkopo wa miaka 3 angalau 40m ili nianze ujenzi na baada ya miaka 2 nifanye top up nichukue tena mkopo so nimejipa miaka 5 niwe nimekamilisha ujenzi. Tukumbuke hao watoto 2 nasomesha kama ada 4m kwa mwaka.
Haya maamuzi ni sahihi ??
Yani umetumia 7mil kupata nyumba? Uli honga?
 
Binafsi sikuoni kama una akili, mkeo kakuacha mbali sana. Kama uliweza honga 7m kupata nyumba nionavyo ungekopa 15m ili uwe na 22m ujenge hizo vyumba 2 ulivyopanga. Baada ya mwaka mmoja wa mmopo ndio ungeanza purukushani za dream house wakati huna presha.

Nakukumbusha wengi hawaanzi na dream [emoji536]. Jifunze kujenga ujue tabia ya ujenzi na baadae uwe nzoefu. Hivi ukifa leo mkeo atabaki na ufahari wa [emoji536] ya NHC?. Vijana wengi wenye kipato mjini huishia kuwa wapangaji wakiwatizama walalahoi wakiishi kwenye nyumba zao kisa mna tamaa ya vitu vizuri bila kujua ugumu wa upatikanaji wake.
 
Binafsi sikuoni kama una akili, mkeo kakuacha mbali sana. Kama uliweza honga 7m kupata nyumba nionavyo ungekopa 15m ili uwe na 22m ujenge hizo vyumba 2 ulivyopanga. Baada ya mwaka mmoja wa mmopo ndio ungeanza purukushani za dream house wakati huna presha.

Nakukumbusha wengi hawaanzi na dream [emoji536]. Jifunze kujenga ujue tabia ya ujenzi na baadae uwe nzoefu. Hivi ukifa leo mkeo atabaki na ufahari wa [emoji536] ya NHC?. Vijana wengi wenye kipato mjini huishia kuwa wapangaji wakiwatizama walalahoi wakiishi kwenye nyumba zao kisa mna tamaa ya vitu vizuri bila kujua ugumu wa upatikanaji wake.
Huko site ilipo ningetumia laki 4 kwa mafuta ya gari kwenda na kurudi ofisini kwa mwezi. Na muda almost 2 hrs x2 za usafiri kuupoteza barabarani. Now nastay 5km kutoka ofisini. Kwa ukaribu huu mara chache sana natumia gari kwenda ofisini .. 3 km wife tumefungua ofisi wife anaisimamia .. 2km shule nzuri ya watoto saa moja watoto wa nursery wanaamka huko wangeamka saa kum na moja saa kumi na 2 xkul bus iwapick. Sasa nadhani unaona value cost ndani ya hizi mishe.
 
Ujinga ni kuhonga 7m ili tu upate nyumba NHC ambayo utailipia kodi 200k kila mwezi, hapo umeokoa nini…. hiyo 7m ingelipa kodi miaka mingapi mtaani jirani na hapo NHC?
Acha mawazo mgando,unadhani ataiacha bure,siju ya kuhama ataiuza pia kurudisha hiyo m7 yake
 
Ujinga ni kuhonga 7m ili tu upate nyumba NHC ambayo utailipia kodi 200k kila mwezi, hapo umeokoa nini…. hiyo 7m ingelipa kodi miaka mingapi mtaani jirani na hapo NHC?
Sehemu ambayo unalipa kodi 200K kwa NHC jua nyumba binafsi zitakuwa mara 2 au 3 ya hio kodi ya NHC.

Wahindi wanakaa kwenye majengo ya NHC ndio maana hawajengi sababu kodi zake ni nyepesi. Mtu binafsi atataka umlipe kodi laki 6 kwa mwezi af kanyumba ka kawaida tu utaweza?

Jamaa yuko sahihi japo huenda kapigwa sana walau angehonga hata 2M ila ndio maisha ya mjini ukiogopa gharama husogei!
 
Kodi ya chini kabisa ya hapa mtaani jirani na nhc ni laki 6 ukipinga kwa mwaka ni milioni 7na laki 2. Hapo bado ishu za ulinzi,usafi ambazo kwa NHC ni ndani ya hyo lak 2... kimsingi kwa hesabu niyoipigaga ya miezi 24 nimeweza kusevu big time. Hapo bado hujaweka ishu ya muda
Mkuu umetumia akili Zako vyema kabisa. Hao wanaokubeza hamna ambaye analipa kodi laki 6 hapo! Wengine wamelala na majaba stoo.

Wengine wanakaa sehemu ambayo kodi laki 3 ila gharama za usafiri na muda ziko juu sana ni sawa na anaelipa kodi laki 6 tu.

NHC kodi ni za kizalendo sana. Watu binafsi wana pangisha nyumba zao ghali sana na usumbufu ni mwingi sana.
 
Mkeo yupo sahihi...wanawake huwa wanawaza hivi..' ukifa yeye ataenda wap? Itakuaje' wanawake wanatuwazia kifo maana mara nyingi wanaona sisi ndio hutangulia..
Pili, mwanamke akiwa kwake anajisikia raha kweli ndio maana wanawake wengi wanakua wa kwanza kuhamia hata kama nyumba haijaisha.
Kwa material uliyonayo, 40m unajenga nyumba nzuri na unahamia, alafu ukianza hizo top up zako ndio ujenge ghorofa lako
Mke wake yupo sahihi ni kweli ila hata mwamba nae hajapuyanga sana. Sababu yeye anampango wa kujenga nyumba ya moja kwa moja na hio nyumba haitaisha haraka namna hio maumivu ya kodi yatakuwa makali ikiwa kodi ni kubwa na gharama ziko juu
 
Back
Top Bottom