Hesabu ya maisha, vipi kwa maamuzi haya nimebugi au iko poa?

Nadhani Mkeo ndie Yuko sahihi,
1: kuhonga 7m ili uanze kulipa kodi ya 200k from 400k sio hesabu kabisa hahaha, gawanya hio 7m kwa laki 2 ambazo unaona ume save, utapata miezi 35. ukimaliza hii ndo utaweza kusema umeokoa gharama... tofauti na hapo laki 2 ulo save kodi ushaihonga.

2:kujenga ni kuzika pesa, USIKOPE KWA AJILI YA KUJENGA unless huo mkopo hauna riba. lakini still bado sio wise decision kukopa ili ukanunue tofali.

Issue nayoona hapa una ego. na hii ndo inaweza kuku cost. curb your ego, fuata ushauri wa mkeo jenga servant qrt hamia.. endelea ujenzi unaotaka polepole bila stress za kodi huku ukisimamia kinachoendelea site mwenyewe
 
Ujenzi hasa nyumba ya kwanza unahitaji umakini wa hali ya juu , kuna vitu vingi hatuvijui kuna hesabu nyingine zipo nje ya makaratasi hyo nyumba unayodhani itagharimu 90 M inaweza kwenda 150 kumbuka sasa hivi nondo na vifaa karibia vyote vya ujenzi vimepanda zaidi ya mara 2 . Yote unayoyawaza yapo sawa lakini kitendo cha kuhonga milioni 7 ili ulipe kodi laki mbili sijaelewa logic yako
 
Yani umetumia 7mil kupata nyumba? Uli honga?
 
Binafsi sikuoni kama una akili, mkeo kakuacha mbali sana. Kama uliweza honga 7m kupata nyumba nionavyo ungekopa 15m ili uwe na 22m ujenge hizo vyumba 2 ulivyopanga. Baada ya mwaka mmoja wa mmopo ndio ungeanza purukushani za dream house wakati huna presha.

Nakukumbusha wengi hawaanzi na dream [emoji536]. Jifunze kujenga ujue tabia ya ujenzi na baadae uwe nzoefu. Hivi ukifa leo mkeo atabaki na ufahari wa [emoji536] ya NHC?. Vijana wengi wenye kipato mjini huishia kuwa wapangaji wakiwatizama walalahoi wakiishi kwenye nyumba zao kisa mna tamaa ya vitu vizuri bila kujua ugumu wa upatikanaji wake.
 
Huko site ilipo ningetumia laki 4 kwa mafuta ya gari kwenda na kurudi ofisini kwa mwezi. Na muda almost 2 hrs x2 za usafiri kuupoteza barabarani. Now nastay 5km kutoka ofisini. Kwa ukaribu huu mara chache sana natumia gari kwenda ofisini .. 3 km wife tumefungua ofisi wife anaisimamia .. 2km shule nzuri ya watoto saa moja watoto wa nursery wanaamka huko wangeamka saa kum na moja saa kumi na 2 xkul bus iwapick. Sasa nadhani unaona value cost ndani ya hizi mishe.
 
Ujinga ni kuhonga 7m ili tu upate nyumba NHC ambayo utailipia kodi 200k kila mwezi, hapo umeokoa nini…. hiyo 7m ingelipa kodi miaka mingapi mtaani jirani na hapo NHC?
Acha mawazo mgando,unadhani ataiacha bure,siju ya kuhama ataiuza pia kurudisha hiyo m7 yake
 
Ujinga ni kuhonga 7m ili tu upate nyumba NHC ambayo utailipia kodi 200k kila mwezi, hapo umeokoa nini…. hiyo 7m ingelipa kodi miaka mingapi mtaani jirani na hapo NHC?
Sehemu ambayo unalipa kodi 200K kwa NHC jua nyumba binafsi zitakuwa mara 2 au 3 ya hio kodi ya NHC.

Wahindi wanakaa kwenye majengo ya NHC ndio maana hawajengi sababu kodi zake ni nyepesi. Mtu binafsi atataka umlipe kodi laki 6 kwa mwezi af kanyumba ka kawaida tu utaweza?

Jamaa yuko sahihi japo huenda kapigwa sana walau angehonga hata 2M ila ndio maisha ya mjini ukiogopa gharama husogei!
 
Mkuu umetumia akili Zako vyema kabisa. Hao wanaokubeza hamna ambaye analipa kodi laki 6 hapo! Wengine wamelala na majaba stoo.

Wengine wanakaa sehemu ambayo kodi laki 3 ila gharama za usafiri na muda ziko juu sana ni sawa na anaelipa kodi laki 6 tu.

NHC kodi ni za kizalendo sana. Watu binafsi wana pangisha nyumba zao ghali sana na usumbufu ni mwingi sana.
 
Mke wake yupo sahihi ni kweli ila hata mwamba nae hajapuyanga sana. Sababu yeye anampango wa kujenga nyumba ya moja kwa moja na hio nyumba haitaisha haraka namna hio maumivu ya kodi yatakuwa makali ikiwa kodi ni kubwa na gharama ziko juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…