Hesabu Za LUKU Zinapigwaje

Hawakati kwenye 4,098.37/=, hiyo 4,098.37/= ndiyo hela yako inayobaki baada kukata kodi (VAT, EWURA, REA) kutoka kwenye elfu 5 yako, kwa hiyo umeme utakaopewa ni wa 4,098.37/= na si wa elfu 5 kamili.
 
Updates
 

Attachments

  • IMG_20241109_163202_395.jpg
    313.5 KB · Views: 2
Ni kwamba kila utakaponunua umeme mfano wa elfu 5 (Tsh. 5,000/=) kuna asilimia inakatwa kwa ajili ya kodi (18.0326% ya pesa taslimu uliyoitoa)

Cha kwanza Kodi (VAT, EWURA, REA) inakatwa kwenye hiyo elfu 5, hiyo kodi ni asilimia 18.0326 (18.0326%) ya hela uliyoitoa ambayo ni 5,000/=

(18.0326%x5000) = 901.63 hii ndiyo kodi ambayo hujumuisha VAT, EWURA, REA.

Kwa hiyo kwenye elfu 5 yako inabaki 4,098.37/= ambayo ndiyo utanunulia umeme.
 
Jamaa amekueleza ukweli halafu we umebisha dah
Alichokuambia ndicho kilivyo

Gharama ya umeme wa unit 14 ndio hiyo 4098

Hiyo 902 no gharama za REA EWERA na VAT

fanya ujumrishe utaona
 
Ieenda sisiemu hiyo kununua ma LC 300
 
Hivi kwa nn Tanwesiko wasilete mfumo ukinunua umeme unaingia moja kwa moja na sio kuweka tena kwenye kile kidude cha mita..inachosha aisee hasa ikitokea uliyemuacha hajui chochote..au umeme umekata usiku hakuna sola betri za remote na PC haina chaji aloo unavurugwa
 
Lakini ukijumlisha COST+VAT+EWURA +REA= 5000 si ina maana elfu tano yako iko accounted for?
 
Jamaa amekueleza ukweli halafu we umebisha dah
Alichokuambia ndicho kilivyo

Gharama ya umeme wa unit 14 ndio hiyo 4098

Hiyo 902 no gharama za REA EWERA na VAT

fanya ujumrishe utaona
shida sio kujumlisha shida ni kwamba kodi ambayo ni 18.0326%,
Mteja kanunua umeme wa 5000
18.0326% of 5000 = 901.63

Hela ilionunua umeme ni 4098.37
[(18% of 4098.37)+(1% of 4098.37)+(3% of 4098.37)] = 901.6414

Hiyo 901.63 kwa nini ilingane?? wakati hizo ni sehemu za hela tofauti au ni coincidence!
ISIJEKUWA IMELINGANISHWA ILI WATU WAKATWE KODI MARA MBILI
 
Hao wanaopinga hoja ya mtoa mada mila maelezo ndiyo wale wale wanajuwa issue ya baltazari na Simba na Yanga tu.
 
Angalia hapo juu unaweza badili hoja yako.
 
Hawakati kwenye 4,098.37/=, hiyo 4,098.37/= ndiyo hela yako inayobaki baada kukata kodi (VAT, EWURA, REA) kutoka kwenye elfu 5 yako, kwa hiyo umeme utakaopewa ni wa 4,098.37/= na si wa elfu 5 kamili.
Hilo wala sio swala la kujadili,
kama unajua kutafuta asilimia fanya kutafuta asilimia ya VAT, EWURA na REA halafu utaona zinapokatwa kama ni kwenye 5000 au 4098.37
 
Mbona hapo Hesabu zpo sawa yaan
Umepewa umeme wa 4098.37 (293/ Unit)
VAT 737.70
EWURA 40.98
REA. 122.95
JUMLA N 5,000.00

 
expand...
shida sio kujumlisha shida ni kwamba kodi ambayo ni 18.0326%,
Mteja kanunua umeme wa 5000
18.0326% of 5000 = 901.63

Hela ilionunua umeme ni 4098.37
kwenye hii hela(4098.37) fanya kujumlisha hela zilizokatwa VAT, EWURA na REA
[(18% of 4098.37)+(1% of 4098.37)+(3% of 4098.37)] = 901.6414

Hiyo 901.63 kwa nini ilingane na jumla ya makato?? wakati hizo ni asilimia(sehemu) za hela tofauti au ni coincidence!
ISIJEKUWA IMELINGANISHWA ILI WATU WAKATWE KODI MARA MBILI
 
Katika mfumo wa LUKU, hesabu zinafanyika kinyume. Wanaanza na jumla (TZS 5,000) na kisha kuhesabu kodi kana kwamba zimetokana na bei halisi ya umeme. Hii ndiyo sababu unaona tofauti kidogo kwenye hesabu.
 
Mfano wa kawaida:

Bei ya soda: TZS 1,000
VAT (18%): TZS 180 (18/100 x 1,000)
Jumla ya kulipia: TZS 1,180 (1,000 + 180)

Tunaanza na bei ya soda, tunahesabu VAT, na kisha tunapata jumla kwa kuongeza VAT kwenye bei ya soda.

Mfumo wa LUKU:

Fikiria unataka kununua LUKU ya TZS 5,000. Badala ya kuanza na bei ya umeme halisi, mfumo wa LUKU unafanya hivi:

Wanaanza na jumla: TZS 5,000 (hii ndiyo kiasi unachotaka kulipia)

Wanahesabu kodi "kinyume": Wanatumia asilimia za kodi (VAT 18%, EWURA 1%, REA 3%) kuhesabu ni kiasi gani cha kodi kinachopaswa kuwemo ndani ya hiyo TZS 5,000.

Wanapata bei halisi ya umeme: Kwa kutoa jumla ya kodi kutoka kwenye TZS 5,000, wanapata bei halisi ya umeme uliyonunua.

Kwa nini wanafanya hivi?
Kuna sababu kadhaa zinazowezekana:

Wanarahisisha hesabu na kuhakikisha kwamba mteja analipa kiasi sahihi (TZS 5,000) kwa umeme pamoja na kodi.

Mfumo wa LUKU umeundwa kuuza umeme kwa njia ya vocha zenye thamani maalum (mfano TZS 5,000, TZS 10,000, nk). Kwa hiyo, wanalazimika kuanza na jumla ya vocha na kisha kuhesabu kodi "kinyume".

Kama Kuna mwenye maoni tofauti na yangu ruksa kuuliza maswali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…