Sema "mtutafutie hela aisee"!Kama tunaanza na kupiga hesabu za LUKU
Tutafute hela aisee
Kama huumizwi na kupigwa kwa wenzako, bado wewe ni mnufaika wa huo uhuni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sema "mtutafutie hela aisee"!Kama tunaanza na kupiga hesabu za LUKU
Tutafute hela aisee
Tuliza wengewashenzi wanapigia asilimia kwenye 4098.37
hapa kuna uwezekano 901.63 ambayo ni sawa na 18.03% inapigwa kila tunaponuna umeme.
Haiingi akilini asilimia zisikatwe kwenye jumla halafu ukijumlisha ije jumla ileile! swali la kujiuliza hiyo hela 901.63Tsh imeenda wapi?
Hesabu rahisi tu jumlisha hiyo 4098.37 na hayo makato,usijitie ujuwaji sana.Hivi wewe unajua kutafuta asililia? tafuta asilimia ya hela ya VAT, EWURA na REA uone zinakatwa kwenye 5000 au 4098.37
Hivi unadhani 1% EWURA 40.98 wamekata kwenye 5000?
hili nalo ni suala la kujadili!
1% of 4098.37 = 40.98
1% of 5000 = 50.00
Kufikia hapo nadhani ushajua VAT, EWURA na REA asilimia zao wanakata kwenye 4098.37
Kuna watu hawajui namna ya kukokotoa hizo hesabu sasa ukijaribu kumuelekeza yeye kazi ni kubisha tu.Mgawanyo wa Gharama
Kwa kawaida, katika ununuzi wa umeme (Luku), kuna gharama za msingi inayojumuisha,
- Gharama halisi ya umeme
- VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) - asilimia 18%
- EWURA levy - asilimia 1%
- REA (Rural Energy Agency) levy - asilimia 3%
Ukokotoaji
Umenunua luku ya shilingi 5,000.00, lakini gharama ya umeme pekee ni 4,098.37.
Gharama hii imechanganywa na asilimia za tozo na kodi zifuatazo.
- VAT (18%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.18 = 737.70
- EWURA levy (1%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.01 = 40.98
- REA levy (3%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.03 = 122.95
Ukijumlisha gharama zote pamoja, unapata jumla ya gharama za umeme na tozo zake, ambazo zinafikia 5,000.00.
4,098.37 + 737.70 + 40.98 + 122.95 = 5,000.00
Sehemu ya shilingi 902 ambayo unasema 'haipo' ni jumla ya VAT, EWURA levy, na REA levy.
737.70 + 40.98 + 122.95 = 901.63
Kwa hiyo, kiasi hiki kinaelekea kwenye kodi na tozo mbali na gharama halisi ya ununuzi wa umeme (yaani, 4,098.37).
Kwa Ujumla:
Matokeo yote haya yanapofikia, ndiyo yanayojumuisha jumla ya 5,000.00 uliyonunua.
- 4098.37 - Gharama ya halisi ya umeme
- 737.70 - Kodi ya VAT (18%)
- 40.98 - EWURA levy (1%)
- 122.95 - REA levy (3%)
Ova