Mgawanyo wa Gharama
Kwa kawaida, katika ununuzi wa umeme (Luku), kuna gharama za msingi inayojumuisha,
- Gharama halisi ya umeme
- VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) - asilimia 18%
- EWURA levy - asilimia 1%
- REA (Rural Energy Agency) levy - asilimia 3%
Ukokotoaji
Umenunua luku ya shilingi 5,000.00, lakini gharama ya umeme pekee ni 4,098.37.
Gharama hii imechanganywa na asilimia za tozo na kodi zifuatazo.
- VAT (18%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.18 = 737.70
- EWURA levy (1%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.01 = 40.98
- REA levy (3%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.03 = 122.95
Ukijumlisha gharama zote pamoja, unapata jumla ya gharama za umeme na tozo zake, ambazo zinafikia 5,000.00.
4,098.37 + 737.70 + 40.98 + 122.95 = 5,000.00
Sehemu ya shilingi 902 ambayo unasema 'haipo' ni jumla ya VAT, EWURA levy, na REA levy.
737.70 + 40.98 + 122.95 = 901.63
Kwa hiyo, kiasi hiki kinaelekea kwenye kodi na tozo mbali na gharama halisi ya ununuzi wa umeme (yaani, 4,098.37).
Kwa Ujumla:
- 4098.37 - Gharama ya halisi ya umeme
- 737.70 - Kodi ya VAT (18%)
- 40.98 - EWURA levy (1%)
- 122.95 - REA levy (3%)
Matokeo yote haya yanapofikia, ndiyo yanayojumuisha jumla ya 5,000.00 uliyonunua.
Ova