Hesabu za matipper ya Mchanga


Kuongezea kwenye Ushauri wa Bongoone, unaweza ukawa na site yako ya Kufyatua tofali. Tipper yako inaweza kuwa inatumika kukuletea mchanga na pia kubeba tofali kupeleka site za wateja. Average site kama uko area nzuri wanahitaji trip 2 au 3 za mchanga kwa siku.

Pia unaweza ukauza kokoto nyeusi za kutoka Msolwa/Lugoba ambazo ndio habari ya mjini kwa sasa. Hapo tayari gari inafanya shughuli yako kwa zaidi ya 70%. Kwa mwenendo huo gari hudumu maisha kwa sababu dereva hana pressure ya kukuletea laki 350,000 kwa siku au 700,000 kwa usiku na mchana.
 
Hii biashara ni ngumu kwa wengi kwa sababu zifuatavyo:

Madereva:
Matajiri wengi wanategemea madereva kwa ushauri juu ya kazi, maintainance etc etc.
Madereva wengi hupenda kazi za uza uza kwa sababu ndio wanapata pesa nyingi hapo.
Kazi za uza uza zina umiza sana gari kama magesabu nilitoa kwepost za awali. Kwamba inabidi atembee trip 4 hadi 5 ili apate pesa yako 300,000/350,000 pesa yake 100,000/200,000 na pesa ya utingo.
Hizi Scania Mende walizi design kubeba mzigo tone 20/24 ikijumlisha uzito wa gari tone 10 ndio inakuwa 32/42 tones.
Sasa hawa madereva inabidi wabdbe mchanga mwingi ili wa wawin wateja hususan wa sites za tofali. Ndio unakuta gari ikikamatwa na watu wa Tanroads inakutwa na 10/15 tones over Manufactures' recommended weight.

Sasa niambie gari lako linabeba uzito huko kila siku na kupita njia zenye makongoro imagine springs, bearings tyres zinakuwa stressed kiasi gani?

Kwa gari za Uza Uza life span yake ni 1 yr kwa huku kwetu, then gari inaanza kuwa member wa garage. Na wewe tajiri unaanza kuwa member wa Tabata Dampo.

Ntawatumia picha ya jirani yangu hapa tipper lake ni reg D lakini liko juu mawe. Madereva wamemtenda vibaya.
 

Ndo maana weng wenye magar maisha yao magumu
Yaan unapata lak nne kwa siku ila kutumia hamsin elfu bar ni vibaya
Kaka nimekuelewa ule siyo mshahara bal ni mauzo yanaweza yakahitaji msing wake
 
Hili somo la sales sio profit ni gumu kweli kwa wajasiriamali wengi
 
Kamanda,,mi natafuta fuso za kukod 2...,ujazo 4cbm, kw dey kila moja ntatoa 100000, matengenezo madogo ni juu yangu..najua kuna matajiri wengi humu wanawapa gari madereva ambao hawana uwezo wa kutunza...mi ntatunza gari mpaka ufurahiii...wenye fuso karibuni...
 
Tupo watu tnaoweza kutunza gari, madereva wa hsb wanaua magar sana...mi nahtaji fuso 2.ambazo ziko order...
 
Ndy mkuu...CBM 4.kama kuna mtu amepaki fuso mpya aniletee mimi nahitaji 2,...usimpe dereva akupe hsb...nipe mimi ...
 
Minatafuta jie fang tipper yenye uwezo Wa kufanya kazi mwenye nayo ani pm
 
Biashara za magari au biashara nyingi inataka kuwa na uzoefu na eneo husika.

Mkuu kuchukua m. 120 na kusubiri hesabu ni risk kubwa sana na ugonjwa wa moyo ful time.

Unaweza kuinvest kwa kupata elimu na uzoefu kwenye eneo fulani , halafu ndio uingie kwenye eneo hilo, ukikuza mtaji na kupanua biashara yako.


Binafsi naona kama unazo M 120 halafu zote unaziweka sehemu ni risk ambayo si calculated na kuhamishia risk, na kutegea majaliwa ya dereva wako tu, hata sikubali kumtegemea dereva tu na hatima yako.
 

Mkuu hapo nilipo bold ndio tumeimba na kuimba. Huwezi kukaa nyumba ni na kutegemea dereva. Wewe mwenyewe unatakiwa kwenda ku lobby na wachina au big contractors kuchukua kazi. Hapo ndio utaona raha ya shughuli. Kwenye hii Industry watu wote waliofanikiwa huwa wa Tender zao sehemu.
 
Ni kweli kabisa.

Bila kutoka na kugonga hodi kwenye maofisi ya watu, biashara za watu hakuna atakayejua upo.

Lakini watanzania hawapendi kabisa kuuza biashara kwa kuogopa rejection ya biashara.

Kama unamwajiri mfanyakazi sector yeyote kwenye kampuni yako, muulize una uzoefu wa sales? atashangaa hadi basi.

Kushangaa kwa nini wakati kila kitu duniani ni salesmanship?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…