mpita-njia
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 1,734
- 1,616
Angalizo tuu wadau sina shaka na mahesabu za magari haswa malori aina ya tipper,tatizo kubwa la biashara hii ni maintanance cost ziko juu sanaa,unaweza pokea hesabu ya miezi mitatu kwa faida lakini mwezi wa nne ikala yote na kukopaaa juu,achilia mbali spare fekii na tabia za madereva wetuu.Udalali pia unachukua sehemu kubwa ya faidaa...au ucheleweshwaji wa malipo..mimi ushauri wangu kama huna mizigo yako mwenyewe by 70% then itakuchukua muda sana kupata matarajio unayo yataka bila kusahau capital intensive ya malori iko juu saanaaa..
Kuongezea kwenye Ushauri wa Bongoone, unaweza ukawa na site yako ya Kufyatua tofali. Tipper yako inaweza kuwa inatumika kukuletea mchanga na pia kubeba tofali kupeleka site za wateja. Average site kama uko area nzuri wanahitaji trip 2 au 3 za mchanga kwa siku.
Pia unaweza ukauza kokoto nyeusi za kutoka Msolwa/Lugoba ambazo ndio habari ya mjini kwa sasa. Hapo tayari gari inafanya shughuli yako kwa zaidi ya 70%. Kwa mwenendo huo gari hudumu maisha kwa sababu dereva hana pressure ya kukuletea laki 350,000 kwa siku au 700,000 kwa usiku na mchana.