NAKUBALIANA ASILIMIA 100 what a hell uache shughuli zoote pengine ndio zilizoleta lori uende kushinda garage na kunafundi alishusha difu kesho yake nikaambiwa kaenda kutengeneza lori Mikumi langu kaliacha.Either that au uwe mtu wa kushinda kwenye ma gereji uswahilini na maduka ya wauza spea used ambazo hata huelewi unauziwa kitu gani. Huko Tabata kwanza gari yako ndogo uliyoenda nayo inaweza kubaki huko huko na yenyewe, kuna hii njia ya kuingilia Tabata kwenye ma spea kutokea Kigogo nilishanusurika kupinduka na SUV, it is so effed up utadhani unaenda maficho ya ISIS. And then mafundi wanadanganya initial estimates za matengenezo, au hajui undani wa tatizo mpaka akishafungua machuma ndio ndio anakwambia kuna hiki na kile na hiki na kile, inabidi u come up na hela ambayo hukuijua toka mwanzo. Kwa kweli biashara za kusimamia mafundi gereji hazina mpango aisee.... kwa hiyo watu wana resort kwenye kuamini watu, kama ulivyosema, which I don't believe in anymore, utafanyaje biashara kwa hesabu za kupewa facts and figures na mtu baki/mwajiriwa? Kuna dereva ashanambia gari imepasuka engine block njiani Mkata, how? The angels know. Na kwamba amefanya kila awezalo akisaidiana na madereva wenzake kuivuta gari kurudi karibu na mji bila ku incur costs za kupeleka spea/mafundi wa kushusha engine maporini huko au kulivuta at a fee, sasa hujui umshukuru ama umfukuze, sina muda kwa kweli wa kwenda Mkata kuhakikisha engine block limepasuka au amefanya change quarter. No way, not again na hizi biashara za kuaminiana.
Watanganyika.
Ukisoma changamoto zangu hapo juu wala usingezungumzia hesabu ya hiyo hela maana kwanza hutaipata madalali nao wanamgao, bila wao kazi haifanyiki na hata hivyo unaweza kwenda kijiweni usiuze huo mchanga. Huko machimboni nako polisi wanachangisha malori bila hivyo hamchoti, pia kuna watu wa rasilimali wana mgao bila kuwasahau kuna mchango sijui wa kijiji yaani ukija kutoa gharama ya mafuta, tingo na dereva ya siku kinachobaki ndio usave in short ni peanut.
Mi napenda challenge lkn za lori kwa kweli ni nyingi mno huwezi kulinganisha na gari zingine ulizotaka kulinganisha. Lori lina kwama porini ambako litakuwa limeharibika pengine na mzigo au limezama. Daladala au taxi hupita kwenye lami lkn siyo malori. Even though kununua lori mtu akuamini umfuatie lori UK hata kwa 50m tu its impractical.