Nimependa Mada hii,napenda kuulizia kuhusu muda ambao Noah inaweza Ikawa fit kufanya kazi in terms ya miaka
Muda ambao Noah inakuwa njiani inategemea na mazingira ya kazi.Inaweze kukaa hata miaka kumi na pia inaweza kukaa miaka miwili tu usiitamani teeeena.
Factors kubwa kwa hizi gari
-Umakini na utunzaji chombo wa Driver,hili unaweza hata wewe kuwa unaikagua,Services ni muhim zaidi
-Njia ambayo gari inaenda yaani routes zake.
Sasa kama ni njia ya lami tupu,basi gari inadum muda mrefu sana
Na kama njia imechongwa ya changarawe nayo pia inadum muda mrefu.
Ila kama njia ni ya mawe utaiuwa muda sio mrefu,zile gari chini hazipendi shurba ya njia mbaya hata kidogo.
Cha kuangalia kwenye route,unafanya kam jinsi daladala,mtakumbuka mliokuwa mnaenda Mabibo miaka ya 1999 jinsi njia ilivyokuwa mbaya,yaani gari zikichoka njia zoote ndiow analeta huko,na ukiangalia gari za Mbezi na Masaki,kama ulaya vile mpaka AC walikuwa wanawawashia abiria wakati ule.
Sasa hizi routes zina classes zake,kulingana na standard ya maisha ya watu,ukiweka route ya Sinza unajua kabisa kwamba Sinza watu wanajipenda sana,sasa kuna siku unawazingua kidogo unawapa AC,au siku mvua ikinyesha unawapa upepo ili kuvutia wateja kwenye gari yako.Biashara siku hizi ujanja tu.
Angalizo kwa wanaoingia kwenye hii Biashara.
Kama ilivyoanza kwenye Bodaboda,suala la kuibiwa,
Biashara hii muda unavyoenda ndio hali inakoelekea kuanza hizi gari kuibiwa.
Nini ufanye,Funga GPRS kwenye Kampuni hata hizi ndogo,itakusaidi ku track gari yako na sio ghali sana kama ni mfanyabisahara makini na unajali milioni zako umezowekeza.Ni bora upate faidia kidogo kwenye biashara iliyo Salama kwako.
Full bima ni muhim pia.