Hesabu za Noah waungwana

Hesabu za Noah waungwana

Hunteroflove

Senior Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
126
Reaction score
92
Nataka kununua Noah, naona naziona nyingi mjini Dar es salaam. Kwa wanaojua hesabu zake kwa hapa mjini Dar es salaam tusaidieni mawazo..
 
Inategemea,inaanzia 30,000 kwa siku mpaka 35,000 kwa siku.Inategemea na Maeneo ambayo na route anazotaka kuhudumia driver wako.
Ila ujue ni aina gani ya Noah iliyo imara kwa kazi hii.

Kuna models nyingi sana za Noah na na ubora haupo sawa.Kuna ambazo shurba kama hizo haziwezi.
Tatizo kubwa la Noah ni kufa mabush, hili ni kwa zote hasa zikiwa zinachukua full seat.

Na pia kuna route zitakubidi ununue 4WD kama itakuwa ni kuingia njia za mchanga au kokoto,ila kwa zile zenye lami moja kwa moja,unaweza kununua hata hizi za kawaida tu sio shida.

Natarajia kuingia kwenye Biashara hiyo mwezi ujao mwishoni,ningekuwa tayari ningekupa mchanganuo na changamoto zake.
Ila nahisi changamoto kwangu hazitakuwa ngum sana maana nazifaham baadhi yake kupitia biashara yangu ya sasa ya Vicarry na bodaboda.Muhim kubwa ni kuhakikisha kwamba gari unaishughulikia hasa pale unapoletewa kesi ndogo,ukiachia tu basi tatizo huzaa tatizo.

Fungua account maalum ya gari lako ili iwe rahisi kwenye kukabiliana na changamoto za dharura. Wengi magari yanawashinda kwa sababu pesa ya gari yeye yoote anaingiza kwenye mambo yake mengine na mwisho wa siku kumuona dereva mbaya.Unakuta inatokea dharura ya engine ku noki basi mtu anakuambia ndani hana hata senti.Na ndio maana mie siku zote huwa nipo Upande wa Madereva kuwatetea,maana sijawahi kukumbana na changamoto za madereva wangu,maana mie ndio ninaeikagua mali zangu na nikiona tatizo hata kama driver hajaliona basi namuambia tulishughulikie.Drivers wachache sana ndio watata na ni rahisi kuwagundua.
 
Ebwana asante sana Zanzibar sasa km unauelewa sehemu gani yenye hesabu hizoo kaka
 
nashukuru na mm nipo njian kuingia kwenye hiyo biashara hasa mkoa na mkoa
 
Nimependa Mada hii,napenda kuulizia kuhusu muda ambao Noah inaweza Ikawa fit kufanya kazi in terms ya miaka
 
Ebwana asante sana Zanzibar sasa km unauelewa sehemu gani yenye hesabu hizoo kaka

Mkuu maeneo mengi sana ya Dar hesabu inakuwa ipo hivyo.Muhim gari iwe nzuri.
Maana abiria wengi wanaangalia gari nzuri,na ikiwa imechoka wanaona ni bora wapande Dalalada tu.
Na unajua kazi hii uzuri wake hata Utingo haina,Driver anasimamia shoo mwanzo mwisho.

Ila kabla hujanunua gari kwanza fanya research,mie yangu niliishamaliza kuifanya zamanis ana,nasubiria wakati tu.

Angalizo kwenye hili,hesabu inaweza kushuka miaka inavyoenda mbele kulingana na ongezeko la gari zenyewe kwenye route husika,ila jingine,hesabu inaweza pia kuwa hivyo muda mrefu kwa kuwa mradi wa mabasi makubwa unakuja na utakuwa na njia maalum.
Noah zina advantages nyingi,moja ni kwamba abiria anashushwa kwenye kituo na wengie wanakuwa hakuna kusimama,wote kwenye siti,hata kama kubanana,na pia route zake zinakuwa sio za kusimama simama hovyo.
Gari ikiwa nzuri unampa dereve mazingira mazuri ya kazi.
Kwenye kazi yoyote inayohusiana na Biashara ya usafiri,wewe kama tajiri hakikisha Driver wako anapenda kazi yake na anapenda gari yako kwa kumtafutia gari nzuri na makorokoro mengine,kama mziki mzuri nk.
 
Nimeyapenda hayo maelekezo ndugu japokuwa sie niliyeuliza ila nimependa hiyo point ya a/c specific ya gari!
 
Nimependa Mada hii,napenda kuulizia kuhusu muda ambao Noah inaweza Ikawa fit kufanya kazi in terms ya miaka

Muda ambao Noah inakuwa njiani inategemea na mazingira ya kazi.Inaweze kukaa hata miaka kumi na pia inaweza kukaa miaka miwili tu usiitamani teeeena.

Factors kubwa kwa hizi gari
-Umakini na utunzaji chombo wa Driver,hili unaweza hata wewe kuwa unaikagua,Services ni muhim zaidi
-Njia ambayo gari inaenda yaani routes zake.

Sasa kama ni njia ya lami tupu,basi gari inadum muda mrefu sana
Na kama njia imechongwa ya changarawe nayo pia inadum muda mrefu.
Ila kama njia ni ya mawe utaiuwa muda sio mrefu,zile gari chini hazipendi shurba ya njia mbaya hata kidogo.

Cha kuangalia kwenye route,unafanya kam jinsi daladala,mtakumbuka mliokuwa mnaenda Mabibo miaka ya 1999 jinsi njia ilivyokuwa mbaya,yaani gari zikichoka njia zoote ndiow analeta huko,na ukiangalia gari za Mbezi na Masaki,kama ulaya vile mpaka AC walikuwa wanawawashia abiria wakati ule.
Sasa hizi routes zina classes zake,kulingana na standard ya maisha ya watu,ukiweka route ya Sinza unajua kabisa kwamba Sinza watu wanajipenda sana,sasa kuna siku unawazingua kidogo unawapa AC,au siku mvua ikinyesha unawapa upepo ili kuvutia wateja kwenye gari yako.Biashara siku hizi ujanja tu.

Angalizo kwa wanaoingia kwenye hii Biashara.
Kama ilivyoanza kwenye Bodaboda,suala la kuibiwa,
Biashara hii muda unavyoenda ndio hali inakoelekea kuanza hizi gari kuibiwa.
Nini ufanye,Funga GPRS kwenye Kampuni hata hizi ndogo,itakusaidi ku track gari yako na sio ghali sana kama ni mfanyabisahara makini na unajali milioni zako umezowekeza.Ni bora upate faidia kidogo kwenye biashara iliyo Salama kwako.
Full bima ni muhim pia.
 
Back
Top Bottom