Heshima kwa bibi Tu Youyou aliyefanikiwa kuvumbua dawa ya kutibu malaria ya Artemisinin miaka 50 iliyopita

Heshima kwa bibi Tu Youyou aliyefanikiwa kuvumbua dawa ya kutibu malaria ya Artemisinin miaka 50 iliyopita

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG11477024913.jpg


VCG11473905327.jpg


Leo tarehe 25 Aprili ni Siku ya Malaria Duniani. Kwa maelfu ya miaka, vita vya binadamu dhidi ya malaria havijawahi kukoma. Katika miaka ya 1960, Bibi Tu Youyou na timu yake hatimaye walivumbua artemisinin yenye ufanisi wa kutibu malaria baada ya kuchunguza mamia ya dawa za jadi za Kichina, kushuhudia wakishindwa mara mia kadhaa, na majaribio ya binadamu pamoja na yeye binfasi. Kwa hivyo, mwaka 2015, Tu Youyou aliyekuwa na umri wa miaka 85 alishinda Tuzo ya Nobel katika Fiziolojia au Tiba.

Katika miaka 50 tangu kuvumbuliwa kwake, dawa ya artemisinin imesaidia China kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria. Wakati huo huo, China imehimiza kikamilifu matumizi ya artemisinin duniani kwa kutoa dawa, msaada wa kiufundi, kusaidia kujenga vituo vya kupambana na malaria, na kutoa mafunzo, na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu katika nchi zinazoendelea.

Rais Xi Jinping wa China katika barua yake ya pongezi kwenye kongamano la kimataifa la maadhimisho ya miaka 50 ya matumizi ya dawa ya artemisinin na kusaidia kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja ya afya, alisisitiza kwamba China inapenda kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa ili kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya ya umma, kufanya kazi pamoja kushughulikia matishio na changamoto za kimataifa, na kukuza kwa pamoja ujenzi wa pamoja wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja ya binadamu na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kulinda afya ya watu katika nchi zote.
 
Artesunate
Artmether
Artmether Lumefantine
Dihydroartemisinin
From sweet wormwood /Artmesia annua
 
Mwanzoni nilikuwa nahisi we ni lichina linalojua kiswahili kumbe ni limatumbi la zanzibar pua nene na midomo hiyo😂😂
 
Back
Top Bottom