HESHIMA KWA TIMU PINZANI/PAKI BASI

HESHIMA KWA TIMU PINZANI/PAKI BASI

babacollins

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
901
Reaction score
212
"Heshima kwa timu pinzani" au "kuwapa heshima wapinzani", mara nyingi kauli hizi hupewa uzito sana na wachambuzi wetu pindi timu ndogo inapokutana na timu kubwa.

Na kwa asilimia kubwa wakimaanisha timu ndogo kucheza mchezo wa kujihami/kupaki basi.
Mpira wa miguu una matokeo matatu na kati ya hayo tokeo lolote linaweza likaihusu timu yoyote zinapokutana timu mbili hivyo heshima nje na ndani ya uwanja inazihusu timu zote.

Timu kujiandaa dhidi ya timu pinzani kwa kuisoma na kuweka mikakati na utekelezaji wa mikakati hiyo nje na ndani ya kiwanja na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kabla na baada ya mchezo kuanza ni miongoni mwa mambo ya msingi katika utekelezaji wa dhana ya kuheshimu timu pinzani.

Ni Mimi Mchezaji kiongozi.
 
Back
Top Bottom