madeinmusoma
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 324
- 387
Fainali ya Euro 2012, hapo Muitaliano ashapigwa bao la nne dakika ya 88 na Juan Mata, Wahispania wote wamejaa katika lango la Italia wanasaka bao la tano. Waitaliano wapo pungufu. Hali hiyo inamfedhehesha Ilker Casillas. anaona fedhea kwa sababu Italia ni Taifa kubwa. Asingependa kuona linahadhirika zaidi mbele ya macho yake. Anamuomba Mshika kibendera amwambie mwamuzi amalize mechi. “Respecto por el Rival, Respecto Por Italia”..."Heshima kwa wapinzani wetu, heshima kwa Waitaliano'. Ghafla mwamuzi anamaliza mechi. Casillas anamkumbatia Mwamuzi wa akiba. Anatembea kwa huzuni kwenda kumkumbatia Buffon. Inatokea mara chache sana! BRAVO ILKER
Sasa kuna kichaa mmoja alikuwa anacheza Chelsea anaitwa Andre Schurrle... Ile nusu fainali ya Brazil na Ujerumani nahodha wa Ujerumani, Mats Hummels akawaambia wenzake wasifunge zaidi ya bao tano ambazo wameshafunga kwa sababu ilikuwa aibu kwa Brazil. Kumbe Schurrle hakusikia. Alikuwa anafanya warm up wakati wenzake wakiongea hayo. Kipindi cha pili kaingia katia kamba mbili ndio zikafika saba. Tena moja alimtungua Cesar kwa roho mbaya sana. Ana roho mbaya sana yule mjukuu wa Hittler....
Na siku Tanzania (Taifa Stars), inafungwa 7 pale Algeria.. MAHREZ alitoa pasi 3 za mwisho.. Baada ya kutoa pasi ya mwisho Kwenye lile goal la 7.. Wenzie wakiwa wanashangilia yeye alikuwa akimtazama Mbwana Samatta kwa jicho la huruma...
Baadaye akawaambia wenzie Sipigi tena pasi yoyote ya mwisho.. Goal 7 zinatosha. NA HII NAIFANYA KWAAJILI YA KULINDA HESHIMA YA HUYO MCHEZAJI WA KITANZANIA ALIYEVAA JEZI NO 10.. Akimaanisha Samatta. Maana MAHREZ alikuwa amezitazama sana clip za Mbwana kabla ya Ile mechi yao ya marudiano..
Ina maana bila uwepo wa Mbwana Samatta Stars Ingekufa goli nyingi sana siku Ile.