Heshima ya kipekee sana iwafikie Wanaume

Dada hapo ulipo agiza barakoa nakuja na sanitizer, umeukonga moyo wangu vilivyo.
 
Ni mwema kila wakati.!
Wakati mwingine kinachotuumiza zaidi siyo tatizo bali ni ile 'attitude toward that problem'..!
Keep that positive attitude alive always!! Hilo nalo litapita salama.!!
Ameen my Dada.Umenipa nguvu na strengths sana sana.Ubarikiwe. Umenifanya nitake jua mambo mengi toka kwako.Nakuheshimu na naheshimu privacy ya mtu ndo Maana sijapenda kuja PM direct, kwani wakati mwingine PM huwa na tafsiri hasi hasa kwenu females mkifuatwa huko.

Kuwa na akili hii siku zote ya kutoa mada chanya na mawazo mazuri itaheshimika humu jf.Ingawa muda wa refresh Upo unaweza jadili funny things.Ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
............hence the reason men die early!............ btw, asante kwa kuapreciate husstle zetu Carleen
 
Sisi wanaume huwa tunapambana sana na sababu kubwa kwanza asili, yani mwanaume tangu enzi za Adamu na Eva tumeumbiwa kupambana, tumeandikiwa tutakula kwa jasho letu hiyo ipo kiasili kabisa, pili huwa kuna kuna external forces nyingi nyingi ikiwa moja ni unategemewa na watu wangapi, pia wanawake nyie pia mnatupa chachu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😀😀😀
Hello murembo depal,the sweetest of my fresh blood!.. toka siku nyingi nilishindwa tamka haya!!
Leo itakuwa wasaa mzuri wa mimi kunena yaliyoujaza moyo wangu!..
Weye ndio ile radha ambayo nilikuwa nikiisubiri kwa udi na uvumba!..
Mwandiko wako unanifanyia nikengeuke zaidi na zaidi!!.. sio tu nimekolea kwenye huba lako bali umenikoleza kwa kolozeo ambalo ni wewe tu mwenye tulizo langu la milele..

Nimejaza kibubu ya kusema juu yako naomba niishie hapo ila nakupenda mfano hakuna!..
Wivu nilionao hata sisimizi akitua kwenye mwili wako napagawa..!
Teta nami uniokoe depal..
I love you..😉
 
Asante sana kulielewa hilo Careen. Hivi ndio umenikumbusha hapa kwamba kumbe wanaume tunabeba matatizo mengi na inatakiwa upambane nayo kila wakati. Na ni kweli umenifikisha mbali sana. Kuna muda nakuwa na matatizo huku hili,kule lile tena yakukatisha tamaa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We @ KENZY Acha hzo jamaa mtoto @ Depal kanielewa mimi unaziba rizk mkali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua chochote kwa mangi hapo nakuja kulipa Dada yngu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepata mixture of feelings nilipokua nasoma hii thread kwanza nimejiskia Huzuni sana kwa sababu muandika thread Carleen kipindi alichopitia mpk kuamua kufikiria upande wetu kiumeni ni kipindi kisicho na maelezo mepesi kuweza kuelezeka,kwa mwanamke kupitia kipindi hicho asee yahitaji huyu mtu apewe pole,naomba nikupe pole Carleen pole sana sweetlove hii ndio dunia yetu tunayoishi hatuna budi kukubaliana na uhalisia wa maisha yetu.

Lakini pia nimefurahi sana na kujiskia raha kwasababu kuna mtu ametambua kuwa wanaume kuna nyakati ngumu sana sana tunapitia ktk haya maisha na ktk mapito hayo jamii haituelewi lkn wapo wengine mpk wanaamua kujinyonga au kunywa sumu kwasababu mizigo bado n mizito na jamii nayo inaendelea kukandamiza vitu Haielewi wala haimuelewi huyu mtu wala sababu zozote atakazotoa.

Leo anatokea mwanamke mmoja anatambua kile wanaume tunachopitia yani inakua n kama Mwanajeshi alietoka vitani IRAQ kakoswa koswa na mabomu,mengine yamempata karudii kilema wengine vipofu Halafu siku ya kurudi anapokelewa pale Airport na watu wengiiiiiiiiiiii wamebeba maua wanamkabidhi na kumwambia "pole baba" "hongera kaka" zile pole si kitu,yale maua si kitu kulinganisha na mapito ya kule Vitani lkn furaha anayoipata huyu mjeshi Haielezeki.

Nataka kusema nini kupitia hii thread yako Carleen kuna mtu yupo mahali sasa hv anapitia wakati mgumu sana lkn kwa kusoma hii thread umempush na kumuongezea life Bars,kama zilikua zmebaki 3 bars sasa hivi mnara umeongezeka zinasoma 9+,amini nakwambia wapo watu wanapambana wenyewe No ndugu no rafiki no Jirani ni yeye na miguu yake,akiumwa analala hapo ndani anajipikia Uji kwa shida mpk anapona Tena na kusimama,Asee Carleen nikwambie kitu dear Friend "Thank You".

Wakati nasoma hii thread yako Background nilikua nimeweka Repeat hizi nyimbo mbili ambazo zote zimetoa shukurani na kum'bariki MAMA,wewe ni mwanamke ambae ni Mama kwa mtoto mwingine,n mama kwa mwanaume yeyote yule na kwa thread yako hii nakupa nyota zote za u Mama Bora

Naomba hizi nyimbo Mbili zikuonyeshe how Thankfull i am...

The First One




The Second One



Wanawake wote mnaotambua umuhimu na Thamani/michango yetu Mungu awabariki sana,sina lakuweza kusema kwa kila mmoja wenu ila natamani mtambue tu Neno 1 kutoka kwangu ASANTE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…