Heslb acheni mizengwe???

Heslb acheni mizengwe???

REAL ACTIVIST

Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
39
Reaction score
5
Bado navuta tafakuri ambayo wakati wote inapelekea nijiulize maswali mengi ambayo kwa bahati mbaya nimekuwa nikishindwa kuyapatia majibu.Mfano wa swali mojawapo la msingi ambalo ni kati ya yale mengineyo kadha wa kadha niliyonayo ni hili hapa,HII TABIA YA ULAFI ULIOKITHIRI YA VIONGOZI WALIOPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA NA KUONGOZA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI YA TANZANIA ITAISHA LINI??.Maofisa wa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni walafi zaidi ya ule ulafi mwingine tunaoufahamu,yaani ni walafi zaidi ya MCHWA.Tabia hii ya ulafi imekuwa ikijidhihirisha katika utendaji wao wa kazi.Ni takribani wiki tatu sasa zimepita tangia wanafunzi wa UDOM waliokuwa wamesimamishwa masomo watume wawakilishi wao HESLB kudai pesa za kujikimu ambazo kwa mujibu wa sheria na talatibu Bodi ilitakiwa iwe imeishawapatia hawa wanafunzi pesa zao tangia mwezi wa oktoba,2012,cha ajabu na cha kusikitisha Bodi akawapa hawa wawakilishi makaratasi yenye majina ya wanafunzi wanaotakiwa kulipwa hizo pesa na kuwaahidi eti baada ya siku mbili pesa zao zitakuwa tayari zimelipwa.Cha ajabu mpaka sasa kimya kimetanda.HESLB wamebwenga pesa za wanafunzi hawa sasa hawajui wapate wapi hizi pesa ndipo wawalipe wahanga hawa wa mgomo(UDOM) mwaka kabla ya ule uliopita.HUU NI ULAFI ULIOKITHIRI.HESLB imejaa mizengwe mitupu na imegeuka kuwa mradi wa kujinufaisha wa kikundi cha maofisa fulani fulani hivi ndani ya serikali.WASOMI NA WANAZUONI WOTE PALE POPOTE MLIPO ZINDUKENI KIFIKRA(DON'T BE CONSERVATIVE).Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika,Ameeeeeeen,Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom