Mnajichanganya ninyi tu bodi wapo vema na hawana shida. Saizi unajisajili kwenye web yao na unaona deni lako halisi. Hawawezi kwenda kwa waajiri wote kufanya update ya makato kwenye salary slip ni kazi kubwa sana. Wewe chukua statement yako online jua deni lako, au fika bodi jua deni halisi baada ya msamaha.
Kwa mfano mimi kwenye statement ya bodi nadaiwa laki 8 tu. Lakini salary slip inaonesha nadaiwa mil 2.5
Kuna jamaa yangu salary slip inasoma mil 1.8 lakini statement ya bodi ilimwambia kamaliza deni. Alipowasiliana nao wakamwambia akachukue clearance certificate. Unapeleka utumishi wanaondoa Deni.
Wanaoshughulika na salary slip na kuingiza na kutoa makato ni utumishi/mwajiri. Ndio maana hata bank wakikulipia deni haliondoki automatically ila wanapeleka uthibitisho utumishi au kwa mwajiri kuwa ume clear wanaliondoa kwenye makato ya mshahara, maana ni hao hao utumishi waliweka hayo makato walipoletewa orodha na bodi.
Bodi kupata waajiriwa ilikuwa inawatafuta kupitia waajiri sio system za serikali kukunasa juu kwa juu. Hii ina maana mwajiri ndiye anaweza kutoa au kupunguza makato pale anapoambiwa na bodi. Sasa bodi haiwezi fanya hii kazi kubwa hivi, wewe unaedaiwa nenda ujue deni lako. Kwanza saizi wamerahisisha ni kuingia kwa web yao unajisajili unaona kila kitu, wanakupa na control number hapo hapo ya kulipia. Wanakupa option yakulipia mpk tigopesa. Mnalalamika hata bila kuwa well informed.
Wapo ambao wameajiriwa baada ya makato kupanda kuwa 15% hao deni lao halipo mbali na ukweli uliopo kwenye salary slip kwa uzoefu wangu na pengine yanalingana kabisa.