hawa bodi kwanza wametudharau kinoma, kwani hakuna mtu mmoja wa Equivalent ambaye amepata au jina lake limekosewa kwenye orodha na wa waombaji waliopata. sisi hii bodi mpya hatuihitaji kwani imeharibu kabisa mfumo wa elimu hapa Tz, hivi hawa hawakusoma kwa njia hii au wote ambao wapo bodi wamesoma kwa Direct Entrance, hapana tunatakiwa tubadilike sisi sio watoto wa Matajiri tukaweza kujilipia ADA.
TUNAOMBA BODI HII UNALOJIITA MPYA IWAFIKIRIE HAWA WANAOTA EQUIVALENT hali mbaya mno, na wengine Sayansi na Walimu sasa mnataka watu gani wapate hiyo mikopo.
kwa mfano DIT wanafunzi wengi wanatoka pale na Diploma kwa hiyo hawa wasipate taifa hili Linapoteza wana-sayansi bila kujijua pale wapo Engineers wengi sana, huo ni mfano tu wa sehemu ambazo zitaathirika kwa kutopata mkopo.
sasa sijui mnataka tufanyaje mtoe mikopo kwa hawa EQUIVALENT, sisi tunasubiri tufungue tu tufike vyuoni ili tujue hatima ya sisi mnaotuita Equivalent.
wadau nashukuru tupo pamoja lazima kieleweke mwaka huu.
Mr. Iringa