Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 876
BODI YA MIKOPO YAZIDI KUWAKANDAMIZA WATANZANIA MASKINI: RAIS WETU TUSAIDIE KATIKA HILI
Anaandika Justus Mbawala, 0753 917802 (Copy And Paste)
Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru sana mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna alivyoweza kusikiliza kilio cha muda mrefu sana cha watanzania maskini kuhusu mzigo mkubwa waliobeba wa kulipa mikopo waliochukua kugharamia elimu ya juu.
Wengi tulipata elimu kupitia mikopo hii. Kilio cha muda mrefu kilikuwa kuondolewa kwa mizigo miwili ya Value Retention fee ya asilimia sita na ile asilimia kumi ya adhabu (penalty) kwa wale wote walioshindwa kuanza kulipa mapema baada ya mwaka mmoja wa kuhitimu. Na ukweli ni kwamba mazingira ya ajira kwa sasa sio rafiki kiasi kwamba mhitimu akaweza kuanza kulipa mkopo baada ya kuhitimu. Wengi wapo mitaani kwa takribani miaka mitano sasa hawajapata kazi maalum.
Mwezi Mei wakati wa sikukuu ya wafanyakazi pale Mwanza, Rais alisikiliza kilio cha wengi cha kuondoa ile asilimia sita. Na baadae tena Bodi iliondoa ile asilimia Kumi ya adhabu. Hivyo katika hesabu za kawaida kabisa ilishaonekana kuwa deni litakalo bakia litalipika. Bodi ya Mikopo iliahidi wanufaika kutulia wakati wao wanafanya mahesabu yao ili ifikapo mwezi Julai 2021 mahesabu mapya ya madeni yatajulikana kuwa baada ya kuondolewa kwa asilimia hizo, deni kiasi gani litabakia.
Ninaandika kuonesha masikitiko yangu kwa bodi ya mikopo na kile kilichoonekana kwangu na naamini wapo watanzania wengine watakuwa wamekutana na mtikisiko huu wa deni jipya. Niwaombe wanufaika wenzangu kupekua taarifa mpya za madeni yenu kwenye website ya bodi. Naomba kutoa maelezo ya takwimu kutokana na kile nilichokiona mimi kwenye deni jipya ambalo limeongezeka tofauti na mategemo licha ya kulipa kwa miaka sita mfululizo.
Januari 2015, mwajiri wangu alipokea hati ya madai kutoka bodi ya mikopo ikimjulisha kuwa aanze kunikata mshahara wangu kama sehemu ya kulipia deni langu. Mwajiri alipopokea hati ile alinifahamisha wakati huo nikiwa naishi Songea. Deni alilopokea kwa wakati ule lilikuwa milioni kumi na sita na nusu na senti zake. Nikaanza kukatwa kwenye mshahara wangu. Ilipofika Januari 2016, mwaka mmoja baadae baada ya kuanza kukatwa, nilienda ofisi za Bodi wakati huo zikiwa pale Mwenge. Nikaomba kujua deni langu lote likoje na kwanini lilifika milioni kumi na sita kama lilivyooneshwa kwenye hati ya mshahara wangu.
Jumatano Januari 6 2016 nikapewa statement yangu. Katika statement ile ilionesha mambo yafuatayo:
Jumla ya shilingi 15,782,500/= nilipewa kama mkopo na bodi kwa muda wa miaka minne mfululizo.
Kulikuwa pia na gharama za ziada kwa mpangilio huu:
Administration fee ilikuwa 157,825/=
Penalty ilikuwa 1,578,250/=
Value retention fee 3, 170,550/=
Jumla ya mkopo mzima pamoja na charges hizo ulikuwa 20,689,752/=
Kwa vile nilianza kulipa mwaka mmoja nyuma, statement hii ilionesha kuwa nilikuwa nimelipa kiasi cha shilingi 609,752/=.
Hivyo kufanya balance ya mkopo kubakia 20,079,373/= hadi Jumatano tarehe 6 Januari 2016.
Swali la msingi likabakia hili, ILE MILIONI KUMI NA SITA NA NUSU WALIYOMPA MWAJIRI WALIIPATAJE?
Deni hili ndilo likawekwa kwenye hati ya mshahara wangu (Salary slip) na kuanza kulitumikia. Nimeendelea na malipo tangu Januari 2015 hadi June 30, 2021. Hivyo basi deni ambalo nimekuwa naishi nalo kwa mwajiri wangu hadi tarehe 30.6.2021 lililopo kwenye salary slip ni shilingi 6, 983,012/=. Maana yake katika kipindi cha miaka sita nimelipa karibu milioni tisa.
Sasa baada ya kauli ya Mheshimiwa Rais kuwa tuondolewe ile asilimia sita na ile asilimia kumi ni matarajio yangu kuwa deni lililopo kwenye hati ya mshahara lingepungua au kubakia lile lile na sio kuongezeka tena.
Tarehe 8.7.2021 niliona niingie kwenye website ya Bodi ili kupata deni langu baada ya marekebisho niliyotarajia. Bodi imeniongezea mzigo mwingine tena badala ya kupunguza mzigo kama nilivyotarajia. Kwenye statement ya tarehe 8.7.2021 bodi ilinipa standing debt mpya kabisa kama ifuatavyo:
Jumla ya mkopo wote kwa miaka minne ni shilingi 15,782,500/=. Mkopo huu upo sawa na ule wa tarehe 6.1.2016 wakati napewa statement.
Makato ya jumla ya kiutawala shilingi 1,266,274 na senti kumi. Charges hizi zimetofautiana na zile nilizopewa tarehe 6.1.2016 kwa kiasi kikubwa sielewi kwanini administration fee imepanda tena.
Hadi tarehe 8.7.2021 bodi inasema nimerudisha jumla ya shilingi 7,485,988/=
Hadi tarehe 8.7.2021 bodi inasema nadaiwa jumla ya shilingi 9,562,786 na senti kumi.
Wakati huo huo kwenye hati ya mshahara wangu deni lililobakia linaonesha kuwa shilingi 6,983,012/=.
Ndugu zanguni hadi hapa unaona kabisa kuwa hesabu hizi ni za mkanganyiko mtupu na kuna mzigo mkubwa umeongezwa kwangu. Nikiwa na matumaini kuwa namaliza deni kumbe bodi imenipa mzigo wa ziada. Siwezi kuumaliza tena kama nilivyodhani. Kuna madai hapa hayapo sahihi. Kuna ongezeko la deni jipya tena la shilingi 2,579,774 na senti 10. Hili ongezeko halijulikani limetokana na nini.
Kwa madai mapya hadi sasa kwa baada ya mheshimiwa rais kusamehe ile asilimia sita na bodi asilimia kumi maana yake nilipaswa kuona deni pungufu na sio onezeko lake.
Mimi naamini mwajiri alipewa deni halali na ndilo ambalo alianza kunikata. Leo hii kwenye salary slip yangu hadi June 30, 2021 nadaiwa kiasi hicho tu cha 6,983,012/=. Kwanini utofauti huu umejitokeza kwangu? Kwanini administration fee imeongezeka tofauti na ile niliyopewa awali?
Bodi mnataka kumwangusha Mheshimiwa Rais katika nia yake njema ya kutuondolea mzigo huu uliotutesa kwa miaka mingi sana.
Naomba deni langu liangaliwe upya na Watanzania wengine pia ambao watakuwa wamekumbana na kadhia hii.
Nawasihi wale wote walionufaika na mikopo hii wafuatilie balance zao kwenye website ya bodi.