CELLULAIRE
Member
- Mar 16, 2016
- 76
- 97
Nichukue fursa hii adhimu kabisa kuwapongezeni watu wazima ambao ni Watendaji wa Bodi ya Mikopo nchini ( HESLB ) kwa kuweza kupoteza muda wenu mwingi, kujadiliana, kuchanganya fikra zenu hadi baadae mkaja na maamuzi ambayo Kwenu mmeona yana Tija ya kuwaumbua wadaiwa sugu wa mikopo na kuweka picha zao siku ya Jumatano ijayo.
Ombi langu kuu kwenu ni moja tu nalo ni kwamba nawaombeni mkishamaliza kuwaambua hao wadaiwa sugu kama akili zenu zilivyowatumeni na mlivyoshauriana basi kwa moyo huo huo pia kesho yake mtuwekee pia na wale Watanzania wachache au hata ikiwezekana mmoja wao ambaye ndiyo Kisababishi kikuu cha Wasomi ambao ni wadaiwa Sugu hao Kutokupata Kazi au kutokuwa na Uwezo wa Kujipatia Vipato kama ilivyokuwa zamani ili nao waweze Kuwalipeni hayo Madeni yenu.
Imenifikirisha mno kama watendaji wasomi wazima wa Bodi ( HESLB ) tena mlienda shuleni kabisa huku wengi wenu mkiwa na Elimu za Bachelors, Masters na PhD's mlikaa kitako kabisa katika vikao vyenu na akili zenu zikawatumeni mje na mkakati huu. Nawaza hivi hiyo Taasisi yenu ingekuwa inakaliwa na watendaji ambao hawana elimu hizo kama zenu hali ingekuwaje au na wao Maamuzi yao yangekuwaje?