HESLB na Utumishi kuna nini kati yenu?

HESLB na Utumishi kuna nini kati yenu?

Mbojo

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
1,593
Reaction score
1,309
Naendelea kupata ukakasi kutoka vyombo hivi viwili. Mwenye mamlaka ya kukata fedha za mtumishi ni mwajiri kwa mkataba maalumu pale inapohitajika.

Nirudi kwenye mada, bodi na utumishi wamewabambikia watumishi madeni ya HESLB. Ukiuliza bodi wanadai hawahusiki na risiti za mishahara, utumishi wanasema kuanzia mwezi wa kwanza 2022, bodi wanakata makato yao moja kwa moja hazina. Sasa swali ni je, madeni yaliyoongezewa mf mtu anadaiwa 530000, na deni kuwa 8753000.

Nani anawajibika? Je uhalali wa taasisi ya kifedha kuingilia mshahara wa mtumishi moja kwa moja bila mwajiri kujua umepitishwaje? Kwa mnaofahamu matatizo haya.yameanza baada ya kuyumba kwa mfumo, je kulikua na shida yakimfumo ama watu walichezea.mfumo.
 
Wajitathmini aisee, wanatubebesha mizigo isiyoyetu
 
Bado kuna shida kubwa, mfano Deni ?walikuwa wanakata 170,000 kila mwezi, lakini mwezi wa mwisho zimebaki 40,000. Wao badala ya kukata hio 40,000 wanakata 170,000 ili eti mtumishi aende kuwadai ofisini!!!

Kwa nini wasikate hio iliyobaki tu? Mbona Benki wanaweza?
 
Back
Top Bottom