Heslb na vocadom wanatutapeli watanzania

Heslb na vocadom wanatutapeli watanzania

Charles Ignatio

Senior Member
Joined
Oct 9, 2010
Posts
133
Reaction score
52
VODACOM (M_PESA Service) Nahoji

Kati yenu Vodacom na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) nani Tapeli? Maana kuna matatizo ambayo yaliyokuwa yakileta sintofahamu kwa waombaji wa mikopo mwaka 2013/14. Na kero hizo ambazo zinaleta shaka ni hizi zifuatazo:-

1. Ukilipa kwa M-pesa kwenda HESLB meseji kutoka vodacom haiji kwa wakati mpaka uwapigie simu jambo ambalo ni usumbufu wa hali ya juu kwa wanafunzi, hakuna sense ya technology inayotumika kuchelewesha hizo messeji.

2. Ukishapata hiyo meseji ambayo ina code(tarakimu za kuingiza wakati wa kusajili kwenye bodi ya Mikopo server ya loan board inasema kuwa hawajatumiwa hiyo meseji kutoka vodacom wanashauri usubirie kwa muda wa saa moja au mawili, la kushangaza ni kwamba unaweza usubiri hadi masaa 24 lakini bado tatizo likawa pale pale, ukiwapigia namba yao ambayo wameiweka( Help Desk Support Number: 022 550 7910) inakuwa busy muda wote na wala haiiti zaidi zaidi inakata.

Ukiwapigia vodacom wanatoa namba zifuatazo:- 0689 100006
0689 100007
0689 100008
0657 200991
0767 664429
kwa ajili ya kupata msaada zaidi kutoka loan board lakini swali la kujiuliza hizo namba mbona hawakuziweka kwenye help desk yako? . Utaambiwa namba unazopiga hazipo isipokuwa namba moja tu ambayo 0689 100006 ambayo inaita kwa muda mrefu bila kupokelewa na mara nyingine kuikata kabisa, ikipokelewa utaambiwa hapa sio Loan Board ila ni chooni, ukihoji zaidi unaambiwa wewe umekwisha tapeliwa.

SWALI JE VODA MNATOA NAMBA ZA UONGO KWA WATEJA, AU KATI YA VODA NA HESLB NANI TAPELI Naomba mtueleze hilo tujue ukweli ,maana kuna watu wamelipa zaidi ya mara moja na bado tatizo ni lile lile!
 
Duuugh...hii sasa kali...unaambiwa laivu ushatapeliwa???.... pole...kuna kitu hapo niongezee...ukienda pale msasani ofisini kwao hawataki kuhudumia first time applicants
 
Duh kazi ipo.....basi kama kuna yoyote anaetoa huduma hii ya kuwajazia watoto HESLB atoe no yake aokoe jahazi watoto wanateseka mtaani mpaka sasa wanashindwa kujua mstakabali wao juu ya HESLB
 
Namshukru mwenyezi mungu mimi nilikamilisha zoezi zima ingawaje kuna changamoto chache tajwa hapo juu nilikumbana nazo.
 
Back
Top Bottom