HESLB pesa za mikopo zinatumika Dodoma.

KALOKAGATHOS

Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
38
Reaction score
6
Kugoma,kuacha kuingia darasani,kuandamana,kujinyonga,kurudi nyumbani,kuuza vitu vya ndani,kuwa chizi,kubomoa benki au kuwapiga mawe viongozi wa chuo ni baadhi ya mambo ya kufanya ili kuhakikisha tunapata mikopo yetu kama ilivyo kawaida,haijalishi kwa njia gani au kwa hali gani,hata kama utaipata ukiwa maiti,lakini ufe na pesa zako mkononi,haiwezekani mpaka leo haieleweki pesa tunapata lini,inamaana HESLB mnataka TUPIKE VIATU TULE?,sio wote ni in-service,wengine bila BOOM maisha hayaendi hapa Chuoni,ndo kusema pesa zinatumika Dodoma?,kwani bajeti ya BUNGE LA KATIBA limetokana na HESLB?,ina maana siku hizi HESLB inadhamini Bunge?,mbona tarehe zinaenda na pesa hazionekani?,je,kama kuna Chuo kikuu chochote ambacho mbali na tetesi za kusaini majina,mapepata mkwanja,naomba niambiwe,ni Chuo gani wemeshapewa hela? na kama kipo,mbona vyuo vingine kama hivi vyetu vya UCHOCHORONI hatujapewa pesa? au ndo kusema pesa zipo ila zimebanwa na hawa MCHWA wa hapa Chuoni?,Huku TEKU ndo kimya kabisa,sijui wanataka tule NGUO?
 
Ud tushapewa...tuliwatishia kugoma
faster pesa imekuja
na ya fild tukianza UE Haijaingia hatuondok
 
Kijana amepiga kelele kwa sauti ya juu siyo kawaida. Hazina fanyeni hima kupeleka fedha HESLB ili wazipeleke vyuoni ili vyuo viwape watoto wetu.
 

mlimani washapewa na hapa MUCE tumesaini mzigo unaingia kesho j3.wanavyuo wa sehemu nyingine kueni na subira ila mumbane loan officer wenu awape taarifa kamili.
 
wewe mwenyewe unakiita chuo chako cha uchochoroni? sasa sisi wapita njia tutakiitaje?
 

Mkuu kwenye bold,nyekundu, mstari hivyo vyuo havitakiwi kupewa mkopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…