KALOKAGATHOS
Member
- Jul 9, 2013
- 38
- 6
Kugoma,kuacha kuingia darasani,kuandamana,kujinyonga,kurudi nyumbani,kuuza vitu vya ndani,kuwa chizi,kubomoa benki au kuwapiga mawe viongozi wa chuo ni baadhi ya mambo ya kufanya ili kuhakikisha tunapata mikopo yetu kama ilivyo kawaida,haijalishi kwa njia gani au kwa hali gani,hata kama utaipata ukiwa maiti,lakini ufe na pesa zako mkononi,haiwezekani mpaka leo haieleweki pesa tunapata lini,inamaana HESLB mnataka TUPIKE VIATU TULE?,sio wote ni in-service,wengine bila BOOM maisha hayaendi hapa Chuoni,ndo kusema pesa zinatumika Dodoma?,kwani bajeti ya BUNGE LA KATIBA limetokana na HESLB?,ina maana siku hizi HESLB inadhamini Bunge?,mbona tarehe zinaenda na pesa hazionekani?,je,kama kuna Chuo kikuu chochote ambacho mbali na tetesi za kusaini majina,mapepata mkwanja,naomba niambiwe,ni Chuo gani wemeshapewa hela? na kama kipo,mbona vyuo vingine kama hivi vyetu vya UCHOCHORONI hatujapewa pesa? au ndo kusema pesa zipo ila zimebanwa na hawa MCHWA wa hapa Chuoni?,Huku TEKU ndo kimya kabisa,sijui wanataka tule NGUO?