HESLB yaja na mpango mpya kwa wasiyorejesha mikopo, waungana na RITA, NIDA na Taasisi za Kibenki kuwatambua kirahisi wadaiwa

HESLB yaja na mpango mpya kwa wasiyorejesha mikopo, waungana na RITA, NIDA na Taasisi za Kibenki kuwatambua kirahisi wadaiwa

Afcon 2027

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
309
Reaction score
579
Bodi ya mikopo(HESLB) imeunganisha mifumo ya kimkakati Kwa ajili ya kuwafikia wanufaika wenye kipato lakini hawajaanza kurudisha mikopo hiyo.

Heslb imeingia makubaliano ya ushirikiano na wakala wa usajili, ufilisi na udhamini(RITA), NIDA na taasisi za kibenki lenye lengo la kuwatambua wanufaika wa mikopo hiyo, wenye kipato na ambao awajarejesha mikopo hiyo ilhali Wana kipato.
---
Akizungumza katika hafla ya kubadilishana hati za ushirikiano kati ya HESLB na wadau hao jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano, Septemba 11, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk Bill Kiwia amesema hadi sasa mikoро inayopaswa kurejeshwa ni Sh600 bilioni.

Mikopo ambayo imeshaiva ni Sh2.1 trilioni na hadi sasa zimerejeshwa Sh1.5 trilioni, kuna kama Sh600 bilioni bado hazijarejeshwa, hivyo kama ilivyo katika kampeni za urejeshwaji mikopo, tumeamua kuunganisha mifumo ili kuwafikia wanufaika wenye kipato waanze urejeshaji," amesema Kiwia.

Vilevile, Kiwia amesema muungano na taasisi hizo unaboresha huduma na urahisi huku Bodi ikitekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo Desemba, 2024 mifumo yote ndani ya Serikali iwe inasomana.

"Kama ilivyo majukumu yetu ya kukopesha na kukusanya mikopo, hivyo hatua hii itaongeza tija kuwafuatilia na kuwafikia wanufaika wote nchi nzima," amesema.

Akitaja majukumu ya taasisi hizo walizoungana nazo akianza na Credit Info ambayo inajukumu la kutunza taarifa za wanufaika wa mikopo kwenye taasisi za kifedha hapa Tanzania. Amesema, hivyo wameshirikiana nayo ili iweze kukusanya na kutunza taarifa za wadaiwa na wanufaika wa mikopo ya HESLB ambapo itasaidia bodi kuwafikia wanufaika hao.

"Kwa upande wa Rita, watahakikisha uhalali wa vyeti vya kuzaliwa na vifo na uombaji wa mikopo, hivyo itaongeza tija katika kazi zetu"

Kwa, Nida amesema watarahisisha kupata taarifa za makazi na mawasiliano ya wanufaika ambao hawajaanza kulipa madeni, hasa wale wenye kipato na wapo kwenye sekta binafsi, ushirikiano na wadau hao umelenga kukuza uchumi kwa kubadilishana taarifa pamoja na kuwafatilia na kuwafikia wanufaika wote.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Deusdedit Buberwa amesema: "Nida jukumu lake ni kushirikiana na HESLB ili kuirahisishia kuwafikia wateja wake na kuwafikia wanufaika ambao hawajaanza kurejesha mikopo ili waanze kulipa.

"Pia, nitoe wito kwa Watanzania wote ambao waliwahi kukopeshwa na Serikali, wawe wazalendo wajitokeze wenyewe waanze kurejesha," amesema Buberwa.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Credit Info Tanzania, Edwin Urasa amesema wako tayari kushirikiana na HESLB katika kufanikisha mchakato mzima wa ukopaji na urejeshwaji mikopo hiyo unafanikiwa.

"Katika kuhakikisha wenzetu wa HESLB wanatoa mikopo kwa wakati basi Rita tumetengeneza mfumo wa kieletroniki ambao unaunganisha kati yetu na bodi kurahisisha wanafunzi kufanya mchakato wa mikopo kwa ujumla,"
 
Tutatumia account za ndugu zetu kufanyia biashara, ile hela inauma, nikubwa na ubaya hivyo vyeti vya degree sijawahi kuvitumia, sijaajiriwa private wala Serikalini nafanya biashara nawalipa kodi wanataka nini tena awa heslb? Au wachukue tu hiyo degree 😂😂
 
Bora niliishiaga form niliona mbali
 
😅😅😅😅Mkataba unasemaj
Hii itawezekana labda kipindi NIDA zipo, sasa kipindi cha kabla ya NIDA utambulisho ulikuwa ni namba ya form 4, na hapakuwa na fingerprint wakati wa kuomba mkopo , hata bank tulizopokelea mikopo hatukuweka fingerprint, sasa NIDA haina msaada kwao kwa sisi wa zamani 😂

Hata hivyo ule mkataba ninao, na hauwapi kabisa mamlaka taasisi yeyote ya kibank kukwapua au kuzuia pesa za mkopaji , labda wampeleke mahakamani, halafu mahakama ndio itoe amri, sio Heslb, na hiyo amri unaweza kuikatia rufaa..,. Hawa wanatutishia nyau, desperate imbiciles 😂
 
Kipato chetu wao kinawahusu nini?
 
1726081265619.jpg
 
Back
Top Bottom