HESLB yaja na mpango mpya kwa wasiyorejesha mikopo, waungana na RITA, NIDA na Taasisi za Kibenki kuwatambua kirahisi wadaiwa

HESLB yaja na mpango mpya kwa wasiyorejesha mikopo, waungana na RITA, NIDA na Taasisi za Kibenki kuwatambua kirahisi wadaiwa

Hao hawajielewi..sisi wengine enzi zetu tunaomba mikopo hakukua na mambo ya nida..watatupatia wapi?
 
Hapa hakuna namna itabidi kulipa tu. Sema wamefanya mambo yao yamekuwa complicated. Nimetoka kufungua account kwenye system yao kwanza hawakuonyeshi deni lako kamili.
Pili naona mwaka 2010/2011 inaelekea eti malipo yalifanyika saut wakati mimi sijawahi kusoma saut na wala sikuwahi kuchaguliwa saut.
Kisha sijui kwa nini wasitengeneza vitu kuwa rahisi, mtu akaweza kupewa control number kama hajaajiriwa kupitia huo mfumo baada ya kufungua account akawa analipa tu.
Mbona control no. Wametoa afisa?
 
Mbona control no. Wametoa afisa?
wametoa wapi mkuu? naomba unipe mwongozo maana mimi leo ndo nmefungua akaunti ila sioni chochote cha maana kwenye akaunti. nilikuwa sina mpango wa kuwalipa ila naona niwalipe tusije sumbuan mbele huko.
 
wametoa wapi mkuu? naomba unipe mwongozo maana mimi leo ndo nmefungua akaunti ila sioni chochote cha maana kwenye akaunti. nilikuwa sina mpango wa kuwalipa ila naona niwalipe tusije sumbuan mbele huko.
Me kwenye account yangu naona wameniwekea control no,ingawa sina mpango wa kuwalipa hilo deni .
 
Bodi ya mikopo(HESLB) imeunganisha mifumo ya kimkakati Kwa ajili ya kuwafikia wanufaika wenye kipato lakini hawajaanza kurudisha mikopo hiyo.

Heslb imeingia makubaliano ya ushirikiano na wakala wa usajili, ufilisi na udhamini(RITA), NIDA na taasisi za kibenki lenye lengo la kuwatambua wanufaika wa mikopo hiyo, wenye kipato na ambao awajarejesha mikopo hiyo ilhali Wana kipato.
---
Akizungumza katika hafla ya kubadilishana hati za ushirikiano kati ya HESLB na wadau hao jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano, Septemba 11, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk Bill Kiwia amesema hadi sasa mikoро inayopaswa kurejeshwa ni Sh600 bilioni.

Mikopo ambayo imeshaiva ni Sh2.1 trilioni na hadi sasa zimerejeshwa Sh1.5 trilioni, kuna kama Sh600 bilioni bado hazijarejeshwa, hivyo kama ilivyo katika kampeni za urejeshwaji mikopo, tumeamua kuunganisha mifumo ili kuwafikia wanufaika wenye kipato waanze urejeshaji," amesema Kiwia.

Vilevile, Kiwia amesema muungano na taasisi hizo unaboresha huduma na urahisi huku Bodi ikitekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo Desemba, 2024 mifumo yote ndani ya Serikali iwe inasomana.

"Kama ilivyo majukumu yetu ya kukopesha na kukusanya mikopo, hivyo hatua hii itaongeza tija kuwafuatilia na kuwafikia wanufaika wote nchi nzima," amesema.

Akitaja majukumu ya taasisi hizo walizoungana nazo akianza na Credit Info ambayo inajukumu la kutunza taarifa za wanufaika wa mikopo kwenye taasisi za kifedha hapa Tanzania. Amesema, hivyo wameshirikiana nayo ili iweze kukusanya na kutunza taarifa za wadaiwa na wanufaika wa mikopo ya HESLB ambapo itasaidia bodi kuwafikia wanufaika hao.

"Kwa upande wa Rita, watahakikisha uhalali wa vyeti vya kuzaliwa na vifo na uombaji wa mikopo, hivyo itaongeza tija katika kazi zetu"

Kwa, Nida amesema watarahisisha kupata taarifa za makazi na mawasiliano ya wanufaika ambao hawajaanza kulipa madeni, hasa wale wenye kipato na wapo kwenye sekta binafsi, ushirikiano na wadau hao umelenga kukuza uchumi kwa kubadilishana taarifa pamoja na kuwafatilia na kuwafikia wanufaika wote.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Deusdedit Buberwa amesema: "Nida jukumu lake ni kushirikiana na HESLB ili kuirahisishia kuwafikia wateja wake na kuwafikia wanufaika ambao hawajaanza kurejesha mikopo ili waanze kulipa.

"Pia, nitoe wito kwa Watanzania wote ambao waliwahi kukopeshwa na Serikali, wawe wazalendo wajitokeze wenyewe waanze kurejesha," amesema Buberwa.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Credit Info Tanzania, Edwin Urasa amesema wako tayari kushirikiana na HESLB katika kufanikisha mchakato mzima wa ukopaji na urejeshwaji mikopo hiyo unafanikiwa.

"Katika kuhakikisha wenzetu wa HESLB wanatoa mikopo kwa wakati basi Rita tumetengeneza mfumo wa kieletroniki ambao unaunganisha kati yetu na bodi kurahisisha wanafunzi kufanya mchakato wa mikopo kwa ujumla,"
Hawataweza lolote
 
Labda wanataka wajaze magereza yote nchini ,vijana wenyewe wamejichokea wapo tu huku wanasubiri ununue bia ,ukitoka kwenda chooni apige hata pafu mbili ,Sasa wa hivyo wataweza kulipa hata laki si kujaza wafungwa magerezani tu
 
Back
Top Bottom