STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,633
- 16,586
Hizbullah: Shambulio la Muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni ni jibu kwa uchokozi wake
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: shambulio la maroketi lililofanywa jana asubuhi kulenga ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel), lilikuwa jibu mwafaka kwa uchokozi wa siku ya Alkhamisi uliofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon.
Sheikh Naeem Qassim ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya habari ya Al Mayadin na akaongeza kwamba, utawala ghasibu wa Kizayuni inapasa ujue kuwa Lebanon si uwanja wa utawala huo kumalizia visasi vyake.
Amesema, msingi inaofungamana nao Hizbullah ni kwamba, itatoa jibu mwafaka kwa uchokozi wa aina yoyote utakaofanywa dhidi ya Lebanon. Na kwa sababu hiyo, jana ilitoa jibu kwa mvamizi kwa maroketi kadhaa.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, Israel inapaswa ijue kwamba Lebanon si uwanja wa utawala huo kumalizia visasi vyake, si mahala pa kutunishia misuli yake, kufanya chokochoko au harakati za majaribio na wala si mahala pa kutimizia ndoto inazowaza akilini mwake. Lebanon ni mahala panapolindwa na kutunzwa.
Sheikh Naeem Qassim
Sheikh Naeem Qassim amefafanua kwa kusema: Sisi tumeshatangaza mara kadhaa kuwa, endapo Israel itafanya uchokozi wowote, tumejiweka tayari kutoa jibu. Hizbullah iko kwenye medani ya mapambano kuilinda Lebanon kwa kujiamini na kwa azma na irada kamili.
Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon ya Hizbullah jana ilitoa taarifa maalum na kutangaza kuwa, katika kujibu mashambulio ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel alfajiri ya kuamkia Alkhamisi katika sehemu za wazi za maeneo ya Al Jurmuq na Ash-Shawaakir, jana asubuhi mnamo saa tano na robo kwa saa za Lebanon brigedi za shahidi Ali Kamil Muhsin na shahidi Muhammad Qassim Tahan za muqawama wa Kiislamu zilishambulia kwa makumi ya makombora ya milimita 122 ardhi zilizo jirani na kituo cha kijeshi cha Wazayuni maghasibu katika mashamba ya Shab'a.../
KIUFUPI HUU MKASA ULIANZA HIVI
Huu mkasa ulianza week iliopita baada ya Meli ya Israel kushambuliwa Israel ikiihutumu Iran ndio imepiga meli yao, Israel tokea mda huo anatishia kuishambulia Iran akiomba Marekani na Uengereza kujiunga na yeye ili kuishambulia Iran, Marekani alisema kuwa anafanya uchunguzi huku Uengereza akilaumu Iran kushambulia meli hio na kusababisha raia wake mmoja kufariki, Iran imejibu kuwa shambulizi lolote litajibiwa vikali sana na kwaharaka, Israel ikaendelea na mikwara kuwa inapanga mashambulizi hayo kufanya pekeake bila ya ushirikiano wa nchi kama Marekani na Uengereza na ikatishia pia kulenga Lebanon na Syria
Wakati huo mda mfupi baada ya kutangaza hivyo yalilengwa makombora mawili kutokea Lebanon kuelekea Israel na yote yalibahatika kupenya coz ilikua kama suprise ambayo hawakutegemea kutokea kipindi hiko, makombora hayo yalijeruhi watu kama watu, Israel hapohapo ilijibu mapigo hayo kuazia mda huo mpaka mpaka usiku wanalenga ktk eneo la mashamba wanayosema mashambulizi hayo yalitokea, Israil ikasema inaonyeshea hayo mashambulizi hayatoki kwa Hizbollah bali yanatoka kwa wapalestina wanaoishi nchini Lebanon, kukawa kimya pande zote, Ijumaa mapema Zililengwa missile 20 kwa pamoja kuelekea Israel ambapo hawakutegemea kama mashambulizi hayo yatafanyika, Hizbullah hapohapo ikatangaza live kupitia mtandao wake kuwa ni wao waliolenga missiles hizo kuelekea Israel wakisema kuwa ni jibu la mashambulizi yaliofanyika Alhamis na wakasema Israel ikishambulia tena ktk ardhi ya Lebanon itajibu haraka na itailenga katika miji zaidi ya Haifa na Tel-Aviv
Israel ikasema mashambulizi hayo wanajua Iran inahusika na Italipa kisasi, mpaka sasa Israel haikujibu iko kimya but imeahidi kuwa italipa kisasi
So mpaka sasa inapanga kulipa visasi viwili Iran na Hizbollah