Baada ya kuona Israel ina uwezo mkubwa wa kudukua mawasiliano ya simu, Hezbollah walichofanya ni kufikia uamuzi wa kununua vifaa maarufu vilivyotumika miaka ya 90 vinavyoitwa "pagers", vinatumia mawimbi wa redio badala ya minara ya simu au internet.
Wasilojua ni kwamba walikuwa wamefanya kosa kubwa sana, Hio ni teknolojia rahisi zaidi kuidukua, kwa wataalam wa mitandao kama Israel ni kama kumsukuma mlevi.
Mossad kitengo cha intelejensia cha Israel walikuwa wameshapata taarifa hii, kilichofanywa ni Mossad kujifanya ni wauzaji wa hizo pagers na kujiweka kwenye mazingira ya kupata hio tenda.
Mossad wakapewa tenda ya kuwauzia Hezbollah pagers bila wao Hezbollah kujua, Mossad alizi modify hizo pagers kunasa mawasiliano, kunasa location na kuweka vilipuzi ndani yake.
Watu wamekuwa wanashangaa Israel inajuaje sehemu yalipo maghala ya silaha za Hezbollah, Kujua sehemu sahihi za kulipua viongozi wa Hezbollah, n.k. ni kwamba tayari mipango yao walikuwa wanaifuatilia kwenye pagers, haikuwa muujiza.
ukishamaliza kuitumia tishu unaitupa kwenye dustbin, ndicho kilichotokea hivi leo, Hizo pagers zimelipuka kwa mpigo zikiwa viunoni na mifukoni.
Rimoti ilipobonywa Israel, pagers zikaanza kulipuka, Takribani wana hezbolah elf 1 waliozibeba muda huo wamepata majeraha, tisa inaripotiwa wamefariki, wengi wamepata majeraha kwasababu milipuko ilisetiwa kwa tahadhari iwe midogo isifikie watu wengine, "reducing" civillian casualities.
Hali hii imefanya uongozi wa Hezbollah kupiga marufuku kutumia pagers na kuteketeza zilizobaki stoo
Your browser is not able to display this video.