Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,411
- 3,712
Tunakuletea sasa taarifa kutoka kwa mazishi ya kamanda mkuu wa Hezbollah, Ibrahim Aqil. Aliuawa katika shambulizi la Israel kwenye viunga vya kusini mwa Beirut siku ya Ijumaa.
Shambulio hilo liliashiria kuongezeka kwa awamu ya sasa ya mzozo wa Israel-Hezbollah, ulioanza tarehe 8 Oktoba. Hivi ndivyo wiki hii imekuwa:
Maandalizi makini yalifanywa kwa ajili ya mazishi ya kamanda wa jeshi la Hezbollah Ibrahim Aqil, huku safu za viti vya plastiki zikiwa zimewekwa mbele ya zulia jekundu.
Sherehe hiyo imefanyika katika kitongoji cha kusini cha Dahiyeh huko Beirut, ngome ya Hezbollah.
Maulamaa wa KiShia waliketi i katika safu ya mbele. Wanaume wengi wamekuja kuomboleza, wamevaa nguo nyeusi, na mikanda ya njano ya Hezbollah shingoni mwao.
Kumpoteza Aqil ni pigo kubwa kwa kundi hilo lenye silaha, baada ya mfululizo wa mashambulizi ya kufedhehesha ya Israel na kulipua vifaa vyao vya mawasiliano vya 'pagers' na simu za upepo.
Naibu katibu mkuu wa Hezbollah Sheikh Naim Qassem alikuwa miongoni mwa waliohudhuria na aliketi mstari wa mbele.
Maulamaa wengi wa Kishia waliovalia vilemba vyeupe pia walijitokeza
BBC

- Siku ya Jumanne, watu 12 waliuawa na maelfu kujeruhiwa baada ya 'pagers' zinazotumiwa na Hezbollah kulipuka nchini Lebanon.
- Siku ya Jumatano, simu za upepo zinazotumiwa na Hezbollah pia zililipuka, na kuua watu 27 na mamia kujeruhiwa.
- Hezbollah iliilaumu Israel kwa mashambulizi hayo. Wakati Israeli ilikataa kutoa maoni, inachukuliwa kuwa inawajibika
- Siku ya Ijumaa, Israel ilisema ilifanya mashambulizi ya anga katika kitongoji cha Dahieh, ngome ya Hezbollah kusini mwa Beirut.
- Hezbollah ilisema Aqil aliuawa katika shambulio hilo. IDF inasema iliua watu kadhaa wakuu ndani ya kundi hilo
- Wizara ya afya ya Lebanon ilisema watu 45, wakiwemo watoto watatu, waliuawa katika shambulio hilo - karibu na mahali ambapo mazishi ya leo yamefanyika.