Hezekiah Ochuka: Mwanajeshi aliyeitawala Kenya kwa saa 6 tu baada ya kutekeleza mapinduzi

Hezekiah Ochuka: Mwanajeshi aliyeitawala Kenya kwa saa 6 tu baada ya kutekeleza mapinduzi

Angalau alitimiza ndoto yake ya kuwa Mkuu wa nchi, japo alionja kwa hayo masaa 6 tu!
 
Jaribio lao lingefanikiwa leo hii pasingekuwa na Chama kinaitwa CCM
Kabisa na vyama vingi vingeingia TZ 1984..Kadego na Maganga walinambia mpango ulikuwa ni kupindua na serikali kuongozwa na raia.Wanajeshi wasingekaa sana madarakani.
 
Huyu Mwamba, mnamo mwaka 1982, alimfurusha Rais Moi Ikulu na akachukua nchi.

Ilikuwa hivi!! Hezekiah Ochuka, alikuwa ni mwanajeshi wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Kenya. Inasemwa alikuwa ni rubani matata sana na mtundu. Mwaka 1982, akiwa kikosi cha anga, aliamua kuteka Airforce One na kuingia Ikulu. Moi akapewa taarifa kuna mjuba ameteka Airforce One. Moi akaona hali si shwari, akatoroshwa mafichoni na walinzi wake waaminifu.

Basi, Mwamba akatinga Ikulu na washikaji zake wachache tu. Inasemekana hata hawakufika au si zaidi ya 5. Alipotinga Ikulu, alikuta mageti yako wazi peupe. Moi katimka kusikojulikana. Basi, Mwamba akaingia Ikulu, akacheki mazingira yapo shwari.


Baadaye akaagiza gari, ikaletwa gari ya rais, akapanda, ikaingia barabarani hadi kituo cha redio. Akashika mic na kulitangazia taifa la Kenya kuwa yeye kuanzia muda huo ndiye Rais wa Kenya. Kwa masaa 6, Kenya ikawa kimya. Majeshi yote na vikosi vya usalama vikawa chini ya amri yake.

Sasa sijui nini kilitokea. Baadaye, vikosi vitiifu viliingia Ikulu kumsaka Rais Hezekiah Ochuka. Jamaa alipoona vikosi vimetinga Ikulu, Mwamba akaiteka tena Airforce One na kupaa angani. Akavuka anga la Kenya na kukimbilia Tanzania. Walimruhusu kutua. Alipotua tu, akadakwa na vikosi vya anga vya Tanzania na kuwekwa rumande.

Baadaye, alirejeshwa Kenya kwa sharti la kubadilishana wafungwa kati ya Kenya na Tanzania. Ikumbukwe hata Mwalimu Nyerere naye alipata adha ya kutaka kupinduliwa. Waliposhindwa wasaliti, walitimkia Kenya na kudakwa na kuwekwa gerezani. Hivyo, Ezekiel alikabidhiwa kwa Moi. Mwaka huohuo, alihukumiwa kunyongwa.
Mkuu maana ya Air Force One sijaielewa.
 
Back
Top Bottom